Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ayatollah Khamenei alijibu madai ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu utayari wake wa kufanya makubaliano na Iran, akisema:
“Rais wa Marekani anasema anataka kufanya Makubaliano na Iran; makubaliano ambayo matokeo yake yamepangwa tayari kwa njia ya vitisho na mabavu siyo makubaliano-bali ni kulazimishwa, na taifa la Iran halitakubali kulazimishwa.”
Ameongeza kuwa Iran haiwezi kushawishiwa wala kutishwa na mbinu za kibabe kama ambavyo mataifa mengine yanaweza kushawishiwa.
Your Comment