Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Hawzat Imam Ridha (a.s) - Chini ya Taasisi ya Kiislamu ya Hujjatul Asr Society of Tanzania - Ikwiriri – Rufiji, Mkoa wa Pwani, inatumia Nafasi hii kuwatangazieni nafasi za masomo ya kidini kwa mwaka wa masomo 2025 – 2026. Waislamu wote wanaopenda kujifunza elimu za dini ya Kiislamu chini ya mwongozo wa Ahlul-Bayt (a.s) wanakaribishwa kuomba nafasi katika Hawzat hii Tukufu.
Tarehe ya Usaili: Jumamosi, 22 Novemba 2025 - Mahali: Makao Makuu ya Hawzat Imam Ridha (a.s), Ikwiriri – Rufiji.
Vigezo vya Mwombaji: Awe ni Muislamu mwenye nia ya dhati ya kusoma elimu za dini. Awe amemaliza angalau elimu ya sekondari (O-Level) au sawa na hapo. Awe tayari kufuata nidhamu na kanuni za Hawza.
Faida za Masomo:
1_Mafunzo ya kidini kwa kina katika mazingira ya kiroho.
2_Miongozo na malezi bora kutoka kwa walimu wenye sifa.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:
📞 Simu: [+255 787 103 888]
Hawzat Imam Ridha (a.s)
“Elimu ni nuru, na nuru hiyo ni ya Allah (s.w.t)”
Your Comment