Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA)- ametoa salamu za rambirambi katika Ubalozi wa Kenya jijini Dar es Salaam, Tanzania, akimfariji Balozi wa Kenya na kuwapa pole wananchi wote wa Kenya kufuatia kifo cha mwanasiasa mkongwe na mashuhuri wa Afrika Mashariki, Baba Raila Amolo Odinga, aliyewahi pia kuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya. Amesema kuwa Watanzania wote wapo pamoja na Wakenya katika msiba huu mzito, na kwamba wote tunaomboleza kwa pamoja, tukimuombea marehemu apumzike kwa amani ya milele.

24 Oktoba 2025 - 00:18

Sheikh Dr.Alhad Mussa Salum: "Poleni Sana Wakenya"

Your Comment

You are replying to: .
captcha