mbinu
-
Barua za Nahjul Balagha - Barua ya 32 | Mbinu za Muawiya, Njia ya Vyombo vya Habari vya Kigeni vya Leo
Mbinu za vyombo vya habari katika kueneza batili na kuunda shubha ili kuwazamisha watu ndani ya fikra zisizo za Kimungu zimekuwa zikitumiwa na wapinzani wa njia ya haki katika vipindi vyote vya historia. Ingawa njia hizi hubadilika kulingana na zama, malengo yao hubaki yale yale. Kurejea mbinu hizi katika mojawapo ya barua za Imam Ali (a.s) kwa Muawiya na kulinganisha na mbinu za vyombo vya habari vya kigeni katika ulimwengu wa leo kunadhihirisha ukweli kwamba “Muawiya na wanaofanana naye” katika historia wamejitahidi kupotosha wengine ili kufikia malengo yao wenyewe-juhudi ambazo hatimaye hupelekea maangamizi yao pamoja na maangamizi ya wale wanaowafuata.
-
Ayatollah Khamenei: Makubaliano ya Mabavu si Makubaliano, Bali ni Kulazimishwa — Iran Haitakubali Kulazimishwa
"Rais wa Marekani anasema anataka kufanya makubaliano na Iran; makubaliano ambayo matokeo yake yamepangwa tayari kwa njia ya vitisho na mabavu siyo makubaliano-bali ni kulazimishwa, na taifa la Iran halitakubali kulazimishwa.”
-
Jenerali Shakarchi: Uzalishaji wa Makombora ya Iran Hautasimama Kamwe / Uzoefu wa Libya Umeonyesha Kuondoa Silaha Kunaleta Uharibifu Tu
Shakarchi aliongeza: Adui walidhani kuwa kuendelea kwa vita zaidi ya wiki moja kutasababisha uchovu na kuchoshwa kwa watu, lakini ushiriki mkubwa wa umma na msaada usiokatizwa kwa Mapinduzi na mfumo viligonga mipango yao yote na mfululizo wa kushindwa kwao ukaendelea.
-
Mwandishi maarufu wa Iraq afichua:
Operesheni za kuzunguka (mbinu za ujanja) kwa mtindo wa Kimarekani; Vita vinavyoitwa amani
"Abbas al-Zaydi", Mwanaharakati wa vyombo vya habari kutoka Iraq, ameandika katika makala yake kwamba: Marekani, kwa jina la amani, inaendeleza vita vyake vya hivi karibuni dhidi ya dunia kwa njia kadhaa, ambazo huenda muhimu zaidi kati ya hizo ni kupitia miungano kama NATO, utawala wa Kizayuni wa Israel, na magenge ya kigaidi.
-
Mpango wa Kubadilisha Paradigm ya Mapinduzi ya Kiislamu; Mbinu ya Ubeberu wa Dunia kwa Ajili ya Kutawala Taifa la Iran
Kikao cha kitaalamu chenye mada ya “Ukosoaji na Uchambuzi wa Mpango wa Kubadilisha Paradigm katika Mapinduzi ya Kiislamu; maana na sababu zake kwa mujibu wa fikra za Imam Khomeini (r.a) na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu” kimefanyika kwa juhudi za Idara Kuu ya Utafiti wa Kiislamu ya Shirika la Utangazaji la Taifa.
-
CNN: "Kwa nini TRUMP analazimisha Dunia iamini kuwa aliharibu vituo vya Nyuklia vya Iran?! Kuna Lengo lipi nyuma ya Uongo wake?!"
Uongo wa Trump ni Taktiki inayojulikana kama: "uongo ukirudiwa mara nyingi huanza kuaminika," ambayo inakusudia kuathiri mtazamo wa umma na hata maamuzi ya kimataifa.
-
Hamas: Dhana ya Netanyahu ya "ushindi kamili" ni ndoto tu
Harakati ya Hamas imesisitiza kuwa upinzani dhidi ya mauaji ya kimbari dhidi ya raia umeanzisha vita vya kuvunja nguvu za adui, ambapo kila siku wanatumia mbinu mpya za uwanjani kumshangaza adui.