26 Agosti 2025 - 17:53
Mpango wa Kubadilisha Paradigm ya Mapinduzi ya Kiislamu; Mbinu ya Ubeberu wa Dunia kwa Ajili ya Kutawala Taifa la Iran

Kikao cha kitaalamu chenye mada ya “Ukosoaji na Uchambuzi wa Mpango wa Kubadilisha Paradigm katika Mapinduzi ya Kiislamu; maana na sababu zake kwa mujibu wa fikra za Imam Khomeini (r.a) na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu” kimefanyika kwa juhudi za Idara Kuu ya Utafiti wa Kiislamu ya Shirika la Utangazaji la Taifa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) – ABNA – kikao hiki kimefanyika kwa kushirikiana na Chama cha Historia ya Kisasa na Mapinduzi ya Kiislamu cha Hawza ya Qom, kwa kuhudhuriwa na Hujjatul-Islam Dkt. Nowruzi, Hujjatul-Islam Dkt. Behruzi Lak, Bw. Shamsiyan na Bi. Rezaei.

Dkt. Hujjati, Mkurugenzi Mkuu wa Utafiti wa Kiislamu wa Shirika la Utangazaji, alisema: “Tunahitaji uimara wa kifikra katika kukabiliana na changamoto zijazo; yaani iwapo Mapinduzi yatajengwa juu ya misingi ya imani, hayatayumbishwa na dhoruba wala shinikizo.”
Aliongeza kuwa matunda ya kikao hiki ni kufikiria kuhusu vipengele vya kimaudhui vya kisiasa na namna ya kuendesha vyombo vya habari katika mazingira ya mabadiliko ya kijamii na kidini.

Hujjatul-Islam Dkt. Nowruzi, mwanachama wa bodi ya wadhamini wa chama hicho cha kitaalamu, alifafanua dhana ya paradigm akisema: “Ni mfumo unaojumuisha misingi yote, malengo, sera, taratibu na mbinu za kutatua matatizo ya kijamii na kisiasa.”
Akaeleza kuwa kubadilishwa kwa paradigm ya Mapinduzi ya Kiislamu kunamaanisha kugeuza malengo na misingi ya Mapinduzi kuelekea mabadiliko makubwa.
Alisema: “Iwapo mabadiliko haya yatakuwa ya ndani ya mfumo wa Mapinduzi, yanakaribishwa; lakini kinachoshinikizwa hivi sasa si cha ndani bali kinashambulia misingi ya Mapinduzi.”

Dkt. Nowruzi aliongeza: “Taarifa ya wanamageuzi wa kisiasa ni madai ya adui, kwani walishindwa kufanikisha malengo yao kupitia vita vikali vya kijeshi (kama vita vya siku 12 vya utawala wa Kizayuni). Sasa wanajaribu kupitia vita laini na mabadiliko ya fikra.”
Alisema ubeberu wa dunia licha ya kuwa na vyombo vya habari na uzoefu mwingi, umeshindwa mbele ya Mapinduzi ya Kiislamu, na kwa kukata tamaa sasa unataka kutumia baadhi ya tabaka za ndani ya jamii kufanikisha malengo yake.

Kwa mtazamo wake, “hii ni vita ya kitambulisho na kimsingi,” ambapo paradigm ya Mapinduzi yenye kuzingatia uadilifu, uhuru, maadili na thamani zake, inapambana na mfumo wa ubeberu tangu mwanzo wa Mapinduzi.

Bw. Shamsiyan, aliyekuwa Rais wa Chuo Kikuu cha Habari, aliwataja waandishi wa taarifa hiyo kuwa ni “watu wasio na upeo” kwa mujibu wa Kiongozi Mkuu, akisema: “Hawakulalamika kwa Marekani, bali walimlaumu kabisa mfumo wa Kiislamu na kudai tuko kwenye mwishilio bila njia ya kutoka.”
Aliongeza kuwa hii ni kuiga maneno ya adui ambaye lengo lake kuu ni kutia taifa la Iran chini ya ubeberu wa dunia.

Bi. Rezaei, mhadhiri wa hawza na chuo kikuu, akirejelea mafundisho ya Mitume, alisema: “Lengo la ujumbe wao ni kumwabudu Mwenyezi Mungu na kujiepusha na mataghuti. Hii haimaanishi kujitenga tu, bali kulingana na Kiongozi Mkuu, haiwezekani tawhidi ikakanyagwa chini ya miguu ya taghut.”
Alisisitiza kuwa imani hii inatengeneza mfumo wa fikra na utawala wa Kiislamu unaotegemea mfano wa Imam na Umma.

Hujjatul-Islam Dkt. Behruzi Lak, mhadhiri wa hawza na chuo kikuu, alisema: “Mapinduzi ya Kiislamu kiasili ni ya kisahihisho (reformative), hayahitaji kubadilishwa paradigm. Yana mbinu na zana za kujibadilisha yenyewe kulingana na nyakati.”
Aliongeza kuwa dunia ya karne ya kumi na tano (Hijria) inakabiliwa na “mgogoro wa maana” kutokana na kuporomoka kwa mfumo wa kimaeneo na kisasa (modernity), hasa miongoni mwa vijana.
Kwa mtazamo wake, changamoto kubwa kwa jamii ni mgogoro huu wa maana, na vyombo vya habari hasa Seda o Sima (radio na TV ya taifa) vinapaswa kuelewa tofauti za kizazi na kushughulika na mustakbali wa imani kwa tafiti makini.

Alisisitiza kuwa “jihad ya kubainisha ukweli” (jihād tabyīn) ni jukumu la wanahawza, wasomi na taasisi za utafiti ili kuelewa mahitaji ya siku zijazo na kutoa taswira na mwongozo wa kistratejia kwa mustakbali.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha