Taifa la Iran
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameipongeza timu ya taifa ya Iran ya mieleka ya Greco-Roman kwa ushindi wao wa ubingwa wa dunia
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya michezo ya nchi yetu ambapo Timu ya Taifa ya mieleka ya “freestyle” na “Greco-Roman” zimefanikiwa kwa pamoja kutwaa ubingwa wa dunia katika mashindano moja.
-
Ilibainishwa katika mkutano na waandishi wa habari:
Maonesho ya Picha 'Siku 12 za Iran' Tukio Kubwa la Simulizi ya Vita, Yataoneshwa Nchini 40
Maonyesho ya Picha ya Kimataifa “Siku 12 za Iran” yenye mada ya Simulizi Halisi ya Vita vya Kulazimishwa vya Siku 12, yanayoratibiwa na Jumuiya ya Amani ya Kiislamu Duniani na Taasisi ya Utamaduni, Sanaa na Utafiti ya Saba, kwa ushirikiano wa Taasisi 21 za ndani na kimataifa, yatafanyika kuanzia tarehe 14 Septemba katika Taasisi ya Sanaa na sambamba na nchi 40 duniani.
-
Mpango wa Kubadilisha Paradigm ya Mapinduzi ya Kiislamu; Mbinu ya Ubeberu wa Dunia kwa Ajili ya Kutawala Taifa la Iran
Kikao cha kitaalamu chenye mada ya “Ukosoaji na Uchambuzi wa Mpango wa Kubadilisha Paradigm katika Mapinduzi ya Kiislamu; maana na sababu zake kwa mujibu wa fikra za Imam Khomeini (r.a) na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu” kimefanyika kwa juhudi za Idara Kuu ya Utafiti wa Kiislamu ya Shirika la Utangazaji la Taifa.
-
Ikiwa hatari itatishia Iran, Wairaq hawatanyamaza kimya
Iran haijaomba msaada kwa makundi ya Muqawama ya Iraq, lakini iwapo wananchi wa Iraq wanahisi kwamba hatari ya kweli inatishia Iran, mashujaa watanyanyuka kutoka katika kila nyumba nchini Iraq na kuiangamiza Marekani na utawala wa Kizayuni.
-
Sayyid Ali Khamenei: "Utawala wa Kizayuni haukufikiria kamwe kupokea mashambulizi kama haya kutoka kwa Jamhuri ya Kiislamu".
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu - Leo akihutubia Taifa la Iran, ametoa ufafanuzi mzuri mno wa matukio yalivyojiri, na kauli imara za kutia moyo kwa wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambazo kwa hakika zimeonyesha mshikamano wa kitaifa, ujasiri, na kukataa kuachia madikteta au nguvu za kigeni na kibeberu kutawala na kuidhibiti Kijeshi Mashariki ya Kati. Pia, kauli za Kiongozi huyu imara na mwenye busara na hekima ya hali ya juu, zinaonyesha msimamo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na mashambulizi ya nje, na kutotetereka katika suala zima la kuifyekelea mbali mikono ya adui yeyote yenye nia ovu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Uungaji mkono wa vijana wa Fatimiyya kwa majeshi ya ulinzi ya Taifa la Iran, katika haramu tukufu ya Mwanamke wa Heshima, Hazrat Fatima Maasumah (sa)
Uungaji mkono Mkubwa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unazidi kuonekana kila Kona ya Dunia katika Operesheni yake ya Ahadi ya Kweli 3.
-
"Watu wenye busara wanaoijua Iran,watu wake na historia yake,hawazungumzi na taifa hili kwa lugha ya vitisho,kwa sababu taifa la Iran halisalimu amri"
"Wamarekani wanapaswa kufahamu kuwa aina yoyote ya uvamizi wa kijeshi kutoka kwao hakika itasababisha madhara yasiyoweza kufidiwa.”
-
Tamko la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) kuhusu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) imesisitiza katika tamko lake kwamba: kuanzisha vita dhidi ya Iran ya Kiislamu ni sawa na kuvamia harem (makao matakatifu) ya Ahlul-Bayt (a.s). Katika hali hii, wanaharakati wote wa haki duniani, hasa mashirika na jumuiya zilizo chini ya mwavuli wa Ahlul-Bayt na wale wanaohusishwa na Jumuiya hii, wanaweza sasa kwa sauti kubwa kuliko wakati wowote kusema wazi kuwa utawala wa Kizayuni ni wa kigaidi na mvamizi. Aidha, taifa la Iran, likiwa limeungana zaidi na thabiti kuliko wakati wowote, litatoa jibu kali na la wazi kwa utawala huu wa kihalifu na muuaji wa watoto.