24 Septemba 2025 - 09:04
''Umoja wa Kitaifa wa Iran ni ule ule wa Tarehe 13 Juni 2009; Wote wanawajibika''

Mheshimiwa Ayatollah Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, usiku huu katika hotuba ya televisheni akiwahutubia watu, aliueleza umoja na mshikamano wa kudumu wa taifa la Iran kuwa ni ngumi ya chuma juu ya kichwa cha adui.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Usiku wa kuamkia leo (tarehe 24 Septemba), Ayatollah Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika hotuba yake iliyorushwa mubashara kupitia Televisheni akiongea na wananchi wa Iran na Ulimwengu kwa ujumla, alieleza kuwa Umoja na Mshikamano wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kama ngumi ya chuma juu ya kichwa cha adui.

Akiweka wazi sababu ya kutokusalimu amri kwa taifa lenye heshima la Iran mbele ya mashinikizo na vitisho vya adui vinavyolenga kuwalazimisha kuacha teknolojia ya kurutubisha urani yenye manufaa makubwa, alisema: "Mazungumzo ambayo Marekani inataka matokeo yake yaamuliwe na kufanyiwa udikteta mapema hayana faida bali yana madhara makubwa."

Mazungumzo ya aina hii, alisema, yanamtia tamaa adui dhalimu ili aendelee na mashinikizo zaidi na hayaondoi tishio lolote kutoka kwa Iran. Hakuna taifa lenye heshima wala mwanasiasa mwenye busara atakayekubali mazungumzo kama haya.

Kuhusu Umuhimu wa Elimu na Vipaji vya Vijana


Katika mwanzo wa hotuba, Ayatollah Khamenei aliwapongeza vijana kwa kuanza mwezi wa Mehr (ambao ni mwanzo wa mwaka wa masomo nchini Iran) na kuwataka viongozi hasa wa Wizara ya Elimu, Wizara ya Sayansi na Wizara ya Afya, kutambua thamani ya vipaji vya ajabu vya vijana wa Iran.

Alitaja mafanikio ya wanafunzi waliopata medali 40 katika mashindano ya kimataifa, pamoja na ubingwa wa dunia katika somo la astronomia, na pia mafanikio ya hivi karibuni ya vijana katika mieleka na michezo mingine.

Kuhusu Shahidi Hassan Nasrallah


Kiongozi huyo pia alitaja kumbukumbu ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, akimwelezea kama hazina kubwa kwa Uislamu, madhehebu ya Shia, na Lebanon, na kwamba urithi wake unaendelea kupitia Hizbullah na harakati nyingine.

''Umoja wa Kitaifa wa Iran ni ule ule wa Tarehe 13 Juni 2009; Wote wanawajibika''

Muhtasari wa Hotuba katika Vipengele Vitatu


Umuhimu wa Umoja wa Taifa la Iran katika vita vya siku 12 vilivyopita na mustakabali wa nchi.

Umuhimu wa teknolojia ya kurutubisha urani (nuclear enrichment).

Msimamo wa Iran dhidi ya Marekani na vitisho vyake.

1. Umoja wa Kitaifa ni Silaha Dhidi ya Adui
Aliuelezea umoja wa taifa kama sababu ya kushindwa kwa adui katika “vita vya siku 12.” Alisema: “Lengo la adui lilikuwa ni kuleta machafuko kwa kushambulia viongozi na watu mashuhuri, lakini watu walijitokeza kwa wingi mitaani, sio dhidi ya serikali, bali kuunga mkono Jamhuri ya Kiislamu na kupinga uvamizi.”

Adui, alisema, alishindwa kuhamasisha watu dhidi ya mfumo wa Kiislamu, na hata mawakala wake walilaumiwa kwa kushindwa.

2. Umuhimu wa Kurutubisha Urani
Ayatollah Khamenei alieleza kuwa kurutubisha urani ni mchakato wa kisayansi wa kubadilisha urani ghafi kuwa mali muhimu kwa matumizi ya nishati, tiba, kilimo, viwanda, na elimu. Iran imefanikiwa kupata teknolojia hii kwa juhudi zake binafsi, licha ya vikwazo na vizingiti vya kimataifa, na sasa ni miongoni mwa nchi 10 duniani zilizo na uwezo huo.

"Hatuna mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia, lakini tumefikia urutubishaji wa asilimia 60, ambao ni mafanikio makubwa."

Alisisitiza kuwa adui hafahamu kuwa Iran si nchi ya kuogopa vitisho, na teknolojia hiyo haiwezi kufutwa kwa mabomu au vitisho.

3. Mazungumzo na Marekani: Ni Hasara Tupu
Kuhusu mazungumzo na Marekani, Ayatollah Khamenei alisema: Marekani inataka matokeo ya mazungumzo yawe kuacha kabisa urutubishaji wa urani. Hili ni udikteta, si mazungumzo ya haki.

Katika miaka ya nyuma, kupitia makubaliano ya JCPOA (maarufu kama Brukseli au Barjam), Iran ilitimiza wajibu wake, lakini Marekani ilikhalifu ahadi zake, ikaondoka katika mkataba huo, na hakuna ahadi iliyotekelezwa.

Hii inaonyesha kuwa kujadiliana na Marekani hakujaleta faida yoyote bali madhara.“Mazungumzo kama haya hayana tija kwa taifa letu bali ni hatari. Hatuwezi kuweka matumaini kwa watu wanaotishia kutushambulia, wanaua viongozi wetu kama Qassem Soleimani, na wanadanganya kila mara.”

Suluhisho ni Kujiimarisha


Ayatollah Khamenei alihitimisha kwa kusema:

“Njia pekee ya kupambana na adui ni kuwa taifa lenye nguvu – kiulinzi, kisayansi, kisiasa na kiuchumi. Ikiwa taifa litakuwa imara, adui hatafikiria hata kutishia.”

Alihimiza kutegemea msaada wa Mwenyezi Mungu, kuzingatia elimu, juhudi za kitaifa, na mshikamano kama misingi ya maendeleo ya kweli.

Nukuu Muhimu:
1-“Taifa la Iran haliwezi na halitakubali kamwe kusalimu amri mbele ya vitisho.”
2-“Mazungumzo ya aina hii ni kutii amri ya adui, si Diplomasia.”
3-“Heshima ya Taifa iko juu ya kila kitu - hatutauza uhuru wetu.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha