Inapendekezwa kusoma Dua ya (......يا مُدَبِّرَ الاُمُورِ ) hali ya kuwa umerukuu, umesujudu, umesimama, umekaa na irudierudie kila sehemu, na isome hata kila siku na iombe Dua hii kwa wingi katika Usiku wa mwisho wa Ramadhani Tukufu.
Sheikh Said Othman: "Imam Ali (a.s) anakumbukwa na Ulimwengu wote wa Kiislamu kuwa yeye ni Shujaa wa Kiislamu, aliyeupigania Uislamu, na kuuhami Uislamu kwa ushujaa wake na ujasiri wake, daima aliutetea uhai wa Uislamu na aliuheshimisha Uislamu kupitia Upanga wake, kama ambavyo Ummul - Muuminina Khadija (s.a) aliuhamia na kuuheshimisha Uislamu kupitia Mali yake".
Katibu Mkuu wa Baraza la Kidunia la Ahlul-Bayt (a.s.) katika hafla ya kuhuisha Usiku wa 21 wa Ramadhani, akiashiria kwamba kutokukubali ndio msingi wa utawala wa Alawi, alisema: Imam Ali (a.s) ni kielelezo cha ulimwengu wa Wanadamu.