23 Machi 2025 - 00:12
Ayatollah Ramezani: Kutokushindwa ndio msingi wa utawala wa Alawi; Imam Ali (amani iwe juu yake) ni kielelezo cha Ulimwengu wa Mwanadamu

Katibu Mkuu wa Baraza la Kidunia la Ahlul-Bayt (a.s.) katika hafla ya kuhuisha Usiku wa 21 wa Ramadhani, akiashiria kwamba kutokukubali ndio msingi wa utawala wa Alawi, alisema: Imam Ali (a.s) ni kielelezo cha ulimwengu wa Wanadamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna -; Ayatollah Reza Ramezani, jioni ya Ijumaa, Machi 21, 2025, katika hafla za kuhuisha Usiku wa 21 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Usiku wa kuuawa Shahidi Imam Ali (a.s), ambayo ilifanyika katika Msikiti wa Safa wa Rasht, alisema: Mikesha ya Lailatul-Qadr ni fursa adhimu ya kuomba msamaha kwenye mlango wa Mwenyezi Mungu.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s) alitaja riwaya ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kuhusu Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuongeza: Kuhifadhi Dini, kuhifadhi nafsi, kuhifadhi ulimi, kudumisha amani, kutowadhuru majirani na kuzingatia marafiki katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kunamfanya mtu kuwa chini ya msamaha na rehema za Mwenyezi Mungu.

Akizungumzia umuhimu na nafasi ya kuihifadhi ulimi alisema: Kuihifadhi ulimi humkinga mtu asitende dhambi 200.

Kwa mujibu wa Ayatollah Ramezani, kwa mujibu wa Riwaya na Hadithi, yeyote atakayeudiriki Usiku wa Kuamriwa (kwa maana: Usiku wa Lailatul -Qdari ambao ni Usiku wa kuamuriwa Hatima ya Mwanadamu) na asisamehewe, basi huyo yuko mbali na Mwenyezi Mungu.

Mwakilishi wa Gilan katika Baraza la Wataalamu wa Uongozi alisema kuwa Hadhrat Ali (A.S) ni kiigizo kamilifu na akasema: Pamoja na kutaja fadhila, kumtukuza na kumsifu Hadhrat Amir al-Mu’minin, Ali (AS), tunapaswa pia kuwa na bidii katika kumuiga yeye kama mfano na kiigizo chetu chema katika matabaka ya maisha ya kibinafsi na ya kijamii.

Akisisitiza juu ya ulazima wa kumjua Kiongozi wa kweli Amirul - Muuminina Ali (AS), alisema: Mbinu, tabia, dira na mtazamo wa Imam Ali (AS) vinapaswa kutiririka na kuenea katika matabaka yote ya maisha yetu.

Ayatollah Ramezani alisema kwamba, kwa bahati mbaya, wakati mwingine tunapotoshwa katika ufafanuzi kuhusiana na Hadhrat Ali (AS) na Maimamu wengine Watwaharifu, na akaongeza: Baadhi ya upotoshaji wa shakhsia wa viongozi wa kidini umesababisha kuwa vigumu kuwafuata kwa vizuri na kwa usahihi katika jamii.

Mwakilishi wa watu wa Gilan katika Baraza la Wataalamu wa Uongozi alisema kwamba Amirul Muuminina Ali (a.s) ndiye kipimo na kiwango katika sekta zote na akasema: Tabia katika maisha ya kibinafsi na ya kijamii inazaa matunda kwa kumuweka Amirul Muuminina, Hazrat Ali (AS) katika maisha yetu kama kigezo na kiigizo chetu.

Ayatollah Ramezani: Kutokushindwa ndio msingi wa utawala wa Alawi; Imam Ali (amani iwe juu yake) ni kielelezo cha Ulimwengu wa Mwanadamu

Akizungumzia rai ya wakubwa wa dini nyinginezo katika kumsifu Imam Ali (AS), amesema: Hadhrat Amirul Muminin (a.s) ana nafasi muhimu na yenye taathira miongoni mwa wakubwa wa dini zote, na wote wameathiriwa naye kwa namna fulani.

Ayatollah Ramezani amesema kuwa Amirul Muuminina Ali (a.s) ni muujiza wa Mwenyezi Mungu na akaongeza kuwa: Zaidi ya Aya 300 zimeteremshwa katika maelezo yanayomhusu Imam Ali (AS).

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS) alisema kuwa Amirul Muuminina Ali (a.s) ndiye mtu wa migogoro na changamoyo zote, na akasema: Amirul Muuminina Ali (a.s) ni suluhisho la changamoto nyingi, migogoro, shida na misukosuko.

Amesema wafuasi na wakubwa wa dini nyinginezo walishangazwa na (adhama au) ukubwa wa Imam Ali (a.s) na kuongeza: Kwa mujibu wa rai na imani za wakubwa wa dini nyinginezo; Katika Mashariki na Magharibi ya dunia, hakuna mtu mwingine aliyeumbwa kama Ali bin Abi Talib (a.s).

Ayatollah Ramezani aliendelea kusema: Muunganiko wa Serikali na uadilifu ulikuwa ni moja ya maajabu ya Imam Ali (a.s).

Mwakilishi wa watu wa Gilan katika mkutano wa wataalamu wa masuala ya uongozi alisema kwamba Amirul Muuminina Ali (a.s) ni kielelezo cha Ubinadamu na akasema: Hazrat huyu, si mtu makhsusi kwa kundi maalum la watu, bali haitakiwi watu wengine kunyang'anywa shakhsia hii, kila mtu anatakiwa afaidike na Hazrat Ali (a.s), kwa sababu yeye ni wa watu wote.

Aliendelea kuelezea mtindo wa utawala wa Imam Ali (a.s) na kuongeza: Uadilifu na utawala wenye mwelekeo wa Haki, ni moja ya maajabu ya usimamizi (na uongozi) wa Imam Ali (a.s).

Ayatollah Ramezani: Kutokushindwa ndio msingi wa utawala wa Alawi; Imam Ali (amani iwe juu yake) ni kielelezo cha Ulimwengu wa Mwanadamu

Kwa mujibu wa Ayatollah Ramezani, Imam Ali (A.S) aliupamba utawala na usimamizi (uongozi) wa jamii. 

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (A.S) ameeleza kuwa, ukweli na uaminifu ni kanuni muhimu zaidi ya utawala wa Imam Ali (a.s) na akasema: Uimara (kutokushindwa), ni Moja ya misingi muhimu ya utawala wa Amirul-Muuminina Ali (a.s).

Akisema kwamba Serikali ya Kidini lazima ifuate kanuni na maadili ya kidini, aliongeza: Licha ya taabu na matatizo yote katika utawala, Amirul Muuminina, Hazrat Ali (A.S) hakushindwa au kurudi nyuma na kutoka kwenye kanuni za Kiislamu na maadili ya Kidini.

Ayatollah Ramezani alisema: Sijamdharau mtu yeyote kwa kumzungumzia Imam Ali (a.s) katika nafasi ya Uimamu wake, na akaongeza: Imam Ali (a.s) hakuwa mtu wa kutokumjali hata adui yake mbaya zaidi katika utawala wake na usimamizi wa Kiislamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha