Lailatul-Qadri
-
Thamani ya Usiku wa Lailatul - Qadri:
Miezi Elfu Moja (1,000) ni sawa na: Miaka 83, na Miezi 3 na Wiki 3 na Siku 3
Hebu fikiria ukifanya ibada zaidi ya moja katika Usiku huu wa Cheo (Lailatul-Qadri) utalipwa thawabu kiasi gani? na Fikiria ukilala katika Usiku huu na ukose kufanya ibada, utapoteza bahati hii kiasi gani katika maisha yako?!.
-
Ibada za kufanya Usiku wa 23 wa Lailatul-Qadri
Inapendekezwa kusoma Dua ya (......يا مُدَبِّرَ الاُمُورِ ) hali ya kuwa umerukuu, umesujudu, umesimama, umekaa na irudierudie kila sehemu, na isome hata kila siku na iombe Dua hii kwa wingi katika Usiku wa mwisho wa Ramadhani Tukufu.
-
Sababu ya Ushujaa na Ujasiri wa Ali bin Abi Talib (a.s)
Sheikh Said Othman: "Imam Ali (a.s) anakumbukwa na Ulimwengu wote wa Kiislamu kuwa yeye ni Shujaa wa Kiislamu, aliyeupigania Uislamu, na kuuhami Uislamu kwa ushujaa wake na ujasiri wake, daima aliutetea uhai wa Uislamu na aliuheshimisha Uislamu kupitia Upanga wake, kama ambavyo Ummul - Muuminina Khadija (s.a) aliuhamia na kuuheshimisha Uislamu kupitia Mali yake".
-
Ayatollah Ramezani: Kutokushindwa ndio msingi wa utawala wa Alawi; Imam Ali (amani iwe juu yake) ni kielelezo cha Ulimwengu wa Mwanadamu
Katibu Mkuu wa Baraza la Kidunia la Ahlul-Bayt (a.s.) katika hafla ya kuhuisha Usiku wa 21 wa Ramadhani, akiashiria kwamba kutokukubali ndio msingi wa utawala wa Alawi, alisema: Imam Ali (a.s) ni kielelezo cha ulimwengu wa Wanadamu.
-
Kauli mbiu: Amani ya Palestina ni Amani ya Tanzania;
Majlis ya Siku ya Kupigwa Upanga Imam Ali (a.s), imefanyika katika Hawza ya Imam Sadiq (a.s), Kigogo, Dar-es-Salam, Tanzania
Maulana Sheikh Hemed Jalala: "Adui Ibn Muljim (laana iwe juu yake), aliyempiga Imam Ali (a.s) kwa upanga wenye sumu kali, alijua kuwa hawezi kupambana na Imam Ali (a.s) akiwa nje ya Msikiti, hivyo akaona mbinu aliyokuwa nayo ni kumuwinda akiwa katika ibada (swala), kwani awapo katika swala huwa mwili wake na hisia zake zinatoweka Duniani, na anazungumza na Mola wake Mtukufu kama vile hayupo Duniani".
-
Marasimu ya kuhuisha Mikesha ya Siku za Lailatul-Qadr itafanyika katika Haram ya Hadhrat Zainab (s.a)
Marasimu (Sherehe) ya kuhuisha Usiku wa Lailatul- Qadr itafanyika kwa muda wa nyusiku tatu katika Madhabahu (Haram) Tukufu ya Hazrat Zainab (s.a).