Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-: Usiku mmoja (1) tu wa Laitatul -Qadri ambao uko ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ni bora zaidi kuliko Miezi Elfu Moja (1,000), au kwa ibara nyingine: Usiku huo ni bora zaidi kuliko Miaka 83, na Miezi 3 na Wiki 3 na Siku 3.
Ukifanya ibada moja tu ndani ya Usiku huu, unahesabiwa kuwa ni sawa umeifanya ibada hiyo kwa muda wa Miaka 83, na Miezi 3 na Wiki 3 na Siku 3.
Hebu fikiria ukifanya ibada zaidi ya moja katika usiku huu wa cheo utalipwa thawabu kiasi gani? na Fikiria ukilala katika usiku huu na ukose kufanya ibada, uutapoteza bahati hii kiasi gani katika maisha yako?!.
Tunamuombba Allah (s.w.t) atujaalie na awajaalie Waislamu wote kuhuisha Usiku huu wa Leo wa 23 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambao ndio Usiku wa Mwisho wa Laitatul _ Qadri.
Your Comment