Ramadhan
-
Thamani ya Usiku wa Lailatul - Qadri:
Miezi Elfu Moja (1,000) ni sawa na: Miaka 83, na Miezi 3 na Wiki 3 na Siku 3
Hebu fikiria ukifanya ibada zaidi ya moja katika Usiku huu wa Cheo (Lailatul-Qadri) utalipwa thawabu kiasi gani? na Fikiria ukilala katika Usiku huu na ukose kufanya ibada, utapoteza bahati hii kiasi gani katika maisha yako?!.
-
Ibada za kufanya Usiku wa 23 wa Lailatul-Qadri
Inapendekezwa kusoma Dua ya (......يا مُدَبِّرَ الاُمُورِ ) hali ya kuwa umerukuu, umesujudu, umesimama, umekaa na irudierudie kila sehemu, na isome hata kila siku na iombe Dua hii kwa wingi katika Usiku wa mwisho wa Ramadhani Tukufu.
-
Ramadhan ni Mwezi ambao dhambi zote zinaunguzwa (zinafutwa) ndani yake
Mja asikose wala asikate tamaa katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani, bali akithirishe kwa wingi kuomba sana maghfira na msamaha kwa Mwenyezi Mungu, kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, na anasamehe dhambi za aina yoyote ile (ispokuwa dhambi ya kumshirikisha).
-
Fadhila za Mwezi Mtukufu wa Ramadhan:
Tusiwe wavivu ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, na tusichoke kuomba Maghfira na Msamaha
Kila kizuri unachokifanya ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ni thawabu.Hata pumzi zetu tunapopumua ndani ya Mwezi huu, hilo linahesabiwa kuwa ni ibada, na hata kulala kwetu na usingizi wetu ndani yake pia ni ibada. Sisi ni wageni wa Mwenyezi Mungu ndani yake.