Thawabu
-
Swala ya Jamaa ni Mkusanyiko wa Kiroho Uliojaa Fadhila za Dunia na Akhera:
Kwa nini Swala ya Jamaa ni mkusanyiko bora kabisa wa kiroho duniani?
Swala ya jamaa ni mkusanyiko wa kifahari zaidi, bora zaidi, safi zaidi, na wa kiroho zaidi duniani. Kwa sababu hiyo, ina fadhila na thawabu nyingi. Kwa kila hatua anayopiga mtu kuelekea swala ya jamaa, huandikiwa thawabu na wema. Na iwapo idadi ya waswaliji itazidi watu kumi, basi hakuna ajuaye kiwango cha thawabu isipokuwa Mwenyezi Mungu tu.
-
Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi kwa mnasaba wa Wiki ya Utetezi Mtakatifu:
"Ushahidi (shahada) ni thawabu ya jitihada za jihadi; iwe katika utetezi wa miaka 8, au katika mapambano ya kishujaa ya siku 12"
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika ujumbe wake kwa mnasaba wa Wiki ya Utetezi Mtakatifu, aliitaja shahada kuwa ni thawabu ya juhudi za jihadi, na alisisitiza juu ya umuhimu wa kujitolea huku katika kukuza mataifa. Vilevile, alieleza yakini yake juu ya ushindi wa haki na umuhimu wa kushikamana na majukumu ya kidini.
-
Thawabu na Faida Kuu za Kuswali Sala ya Jamaa | Madrasat Hazrat Zainab (sa) Kigamboni, Dar-es-Salam kama mfano hai katika kudumisha Sala za Jamaa
Sala ya Jamaa ni Kinga dhidi ya Shetani. Na Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) alisema: فإنَّما يأكلُ الذئبُ منَ الغنمِ القاصيةَ / “Hakika mbwa mwitu humla Kondoo aliyejitenga.”
-
Thamani ya Usiku wa Lailatul - Qadri:
Miezi Elfu Moja (1,000) ni sawa na: Miaka 83, na Miezi 3 na Wiki 3 na Siku 3
Hebu fikiria ukifanya ibada zaidi ya moja katika Usiku huu wa Cheo (Lailatul-Qadri) utalipwa thawabu kiasi gani? na Fikiria ukilala katika Usiku huu na ukose kufanya ibada, utapoteza bahati hii kiasi gani katika maisha yako?!.