Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
Mwaka huu, Wiki ya Utetezi Mtakatifu imepata mwonekano na adhama nyingine kwa sababu ya kufa shahidi kwa kundi la Mashujaa wakuu wa njia ya Muqawama (Mapambano ya Kiislamu) na vijana jasiri katika maeneo mbalimbali.
Shahada ni thawabu ya juhudi za jihadi - iwe ni katika utetezi wa miaka 8, au katika mapambano ya kishujaa ya siku 12, au huko Lebanon, Gaza, na Palestina. Mataifa hukua kwa juhudi hizi za kujitolea, na hupata Mwangaza na uzuri kwa sababu ya Mashahidi hawa.
Kilicho muhimu ni kuwa na yakini juu ya ahadi ya Mwenyezi Mungu kuhusu ushindi wa haki na kuangamia kwa batili (udhalimu), na kudumu katika kutekeleza wajibu wetu wa kunusuru dini ya Mwenyezi Mungu.
Sayyid Ali Khamenei
24 Septemba, 2025.
Your Comment