siku 12
-
Jeshi la Mapinduzi la Kiislamu la Iran (IRGC):
Hadithi ya vita vya siku 12 iwe kipaumbele kwa wachapishaji na waandishi
Jeshi la Mapinduzi la Kiislamu (IRGC) limeweka mkazo: Moja ya matukio makuu na yenye mafundisho muhimu katika historia ya kisasa, ambayo inaweza kuwa kipaumbele kwa wachapishaji na waandishi wenye ujuzi na uwezo wa nchi, ni Ulinzi Mtakatifu wa siku 12 dhidi ya vita vya kigaidi vilivyofanywa na muungano wa Marekani, utawala wa Kizayuni, na wafuasi wao wa Magharibi na wa kikanda.
-
Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) wa Mkoa Mkuu wa Tehran:
“Vikosi vya ulinzi vya Iran vimewashinda majeshi ya NATO katika vita vya siku 12”
Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) wa Mkoa Mkuu wa Tehran amesema: “Katika vita vya kujihami vya siku 12, tulisimama dhidi ya Marekani, utawala wa Kizayuni na jumla ya majeshi ya NATO. Kwa hakika, tuliwashinda wote wa NATO, jambo ambalo halijawahi kutokea.”
-
Vifo vya Wapalestina 453, wakiwemo watoto 150, vimeripotiwa kutokana na njaa na utapiamlo huko Gaza
Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa idadi ya waathirika waliopoteza maisha kutokana na njaa na utapiamlo imefikia watu 453, ambapo miongoni mwao wako watoto 150.
-
Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi kwa mnasaba wa Wiki ya Utetezi Mtakatifu:
"Ushahidi (shahada) ni thawabu ya jitihada za jihadi; iwe katika utetezi wa miaka 8, au katika mapambano ya kishujaa ya siku 12"
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika ujumbe wake kwa mnasaba wa Wiki ya Utetezi Mtakatifu, aliitaja shahada kuwa ni thawabu ya juhudi za jihadi, na alisisitiza juu ya umuhimu wa kujitolea huku katika kukuza mataifa. Vilevile, alieleza yakini yake juu ya ushindi wa haki na umuhimu wa kushikamana na majukumu ya kidini.
-
Waumini wa Kabul Waadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (a.s) Wakihoji Vikwazo vya Safari za Mahujaji (Mazuwwari) wa Afghanistan
Sambamba na kuwadia kwa siku ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s), hafla ya kuadhimisha siku hii ilifanyika katika Kituo cha Fiqhi cha Maasemamu Watakatifu (a.s) upande wa magharibi mwa jiji la Kabul. Washiriki, sambamba na kufanya maombolezo kwa ajili ya Imam Hussein (a.s), walitoa malalamiko makali dhidi ya ukosefu wa uratibu wa kisiasa na kisheria ambao mwaka huu uliwazuia waumini wengi wa Afghanistan kusafiri kwa wingi kwenda Karbala.
-
Jeshi la Mapinduzi la Iran Laonya Marekani na Israel: Jibu Litakuwa Kali Mno Kuliko Mnavyodhani
Iran iko tayari kwa Operesheni Kubwa Dhidi ya Wachokozi kwa muda wowote ule.