Hujjatul-Islam wal-Muslimin Basim Al-Shar’i amesema kuwa hatari kuu kwa Jamhuri ya Kiislamuinatokana na mambo ya ndani, na akaongeza: “Nguvu ya wananchi wa Iran imo katika umoja wao na kushikamana kwao na uongozi wenye busara wa Ayatullah Khamenei. Umoja huu ndio heshima na mtaji halisi wa Jamhuri ya Kiislamu.”
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika ujumbe wake kwa mnasaba wa Wiki ya Utetezi Mtakatifu, aliitaja shahada kuwa ni thawabu ya juhudi za jihadi, na alisisitiza juu ya umuhimu wa kujitolea huku katika kukuza mataifa. Vilevile, alieleza yakini yake juu ya ushindi wa haki na umuhimu wa kushikamana na majukumu ya kidini.