25 Desemba 2025 - 16:56
Waziri Mkuu Dr. Mwigulu Nchemba: Mgawanyiko na Vita vya Ndani Havina Mshindi, Amani Ndiyo Ushindi wa Taifa

Kupitia salamu zake za Krismas - Waziri Mkuu ameutanabahisha Umma wa Watanzania dhidi ya Mgawanyiko na kusisitiza umuhimu wa Amani.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Mwigulu Nchemba, amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa, akisisitiza kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe pamoja na migawanyiko ya ndani havina mshindi.

Waziri Mkuu Dr. Mwigulu Nchemba: Mgawanyiko na Vita vya Ndani Havina Mshindi, Amani Ndiyo Ushindi wa Taifa


Akizungumza katika salamu zake za Sikukuu ya Krismasi, Waziri Mkuu amesema kuwa vita yoyote inayohusisha wananchi wa taifa moja husababisha hasara kwa pande zote bila mshindi, huku mgawanyiko wa kijamii na kisiasa ukiwa na matokeo ya kushindwa kwa taifa zima.
“Amani ina manufaa makubwa kwa maendeleo ya taifa, lakini kupotea kwa amani kunaleta madhara yasiyokuwa na mshindi,” amesema Dr. Mwigulu Nchemba.

Waziri Mkuu Dr. Mwigulu Nchemba: Mgawanyiko na Vita vya Ndani Havina Mshindi, Amani Ndiyo Ushindi wa Taifa

Waziri Mkuu amehitimisha kwa kuwatakia Wakristo wote nchini Tanzania heri ya Sikukuu ya Krismasi, huku akiwahimiza Watanzania wote, bila kujali tofauti zao za kidini au kijamii, kushikamana katika kujenga taifa lenye umoja, mshikamano na ustawi wa pamoja.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha