Ayatollah Sayyid Yasin Musawi, Imamu wa Ijumaa wa Baghdad na mmoja wa wasomi mashuhuri wa Hawza ya Najaf Ashraf, amesisitiza kuwa “tukio muhimu zaidi duniani kwa sasa ni kusalimu amri kwa Israel na Waziri Mkuu wake Benjamin Netanyahu pamoja na Rais wa Marekani Donald Trump mbele ya masharti ya Muqawama wa Kiislamu huko Gaza.”
Amesema kuwa usitishaji mapigano uliotangazwa hivi karibuni ni “ushindi wa wazi wa Muqawama na matokeo ya uimara wa wananchi wa Palestina.”
"Zainab Basri alisema: Baadhi ya wanasiasa wa Kurdistan ya Iraq, na kwa ujumla makundi ya kisiasa yanayohusiana na Marekani na nchi za Kiarabu za Ghuba, hawapendezwi na uhusiano wa Iraq na Iran..."