24 Desemba 2025 - 16:47
Sheikh Dr.Alhad Mussa Salum | Cheti cha Heshima Kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Kassim Majaliwa ni Taswira Halisi ya "Falsafa ya Upendo na Umoja wa Kudumu"

Kulinda na kuendeleza upendo na umoja ni jukumu la kila mwanajamii - kwa maneno, kwa matendo na kwa maamuzi - ili kujenga mustakabali wenye matumaini, mshikamano na heshima kwa utu wa binadamu.

Sheikh Dr.Alhad Mussa Salum | Cheti cha Heshima Kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh.Kassim Majaliwa ni Taswira Halisi ya "Falsafa ya Upendo na Umoja wa Kudumu"

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Upendo na Umoja ni misingi mikuu ya maisha ya jamii yenye Amani, mshikamano na maendeleo. Upendo huunganisha nyoyo, huondoa chuki na kinyongo, na hujenga daraja la uelewano kati ya watu tofauti. Umoja, kwa upande wake, huimarisha nguvu ya pamoja na kuifanya jamii iwe imara mbele ya changamoto.

Upendo wa kweli haupimwi kwa maneno pekee, bali kwa vitendo vya huruma, kujali, kusameheana na kusaidiana. Vivyo hivyo, Umoja wa kweli haujengwi juu ya maslahi binafsi au ya muda mfupi, bali juu ya misingi ya haki, heshima na dhamira ya pamoja.

Upendo na Umoja havipaswi kuwa vya msimu au kulingana na mazingira, bali viwe ni thamani endelevu zinazodumu kizazi hadi kizazi. Jamii inayojengwa juu ya upendo na Umoja wa kudumu huweza kushinda migogoro, kujenga amani ya kweli, na kusonga mbele kimaendeleo bila kuacha yeyote nyuma.

Kwa hiyo, kulinda na kuendeleza upendo na umoja ni jukumu la kila mwanajamii - kwa maneno, kwa matendo na kwa maamuzi - ili kujenga mustakabali wenye matumaini, mshikamano na heshima kwa utu wa binadamu.

Falsafa ya Upendo na Umoja wa Kudumu

Mwenyekiti JMAT-TAIFA - Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum akimkabidhi Cheti cha Pongezi Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Mheshimiwa Kasaim Majaliwa Majaliwa, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake mkubwa katika Harakati za Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Ujenzi wa Taifa kwa Ujumla.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha