Mufti awataka Watanzania kutumia elimu na teknolojia kujenga nchi na kuleta maendeleo.Akemea matumizi mabaya ya mitandao kuvuruga amani na kuvunja heshima za watu na viongozi. Awataka vijana kuwa makini na watu wanaotumia teknolojia kueneza kashfa na dharau. Asisitiza umuhimu wa kulinda umoja, utulivu na mshikamano wa Watanzania.
"Tuepuke upepo mbaya unaosambazwa kwa chuki za kidini. Sisi Waislamu hatukatazwi kuishi kwa wema na wasiokuwa Waislamu. Maisha ya watu lazima yalindwe,” alisema Mufti.