Makombora
Sheikh Naderi alisema kuwa kwa mujibu wa maelekezo ya uongozi wa juu, kipindi hiki kimepewa jina la *“Wiki ya Ujasiri wa Makombora”* kwa lengo la kuenzi mashahidi na kuonyesha mafanikio ya kikosi hicho kwa wananchi.
Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika ujumbe wake kwa mnasaba wa Wiki ya Utetezi Mtakatifu, aliitaja shahada kuwa ni thawabu ya juhudi za jihadi, na alisisitiza juu ya umuhimu wa kujitolea huku katika kukuza mataifa. Vilevile, alieleza yakini yake juu ya ushindi wa haki na umuhimu wa kushikamana na majukumu ya kidini.