19 Machi 2025 - 15:15
Marasimu ya kuhuisha Mikesha ya Siku za Lailatul-Qadr itafanyika katika Haram ya Hadhrat Zainab (s.a)

Marasimu (Sherehe) ya kuhuisha Usiku wa Lailatul- Qadr itafanyika kwa muda wa nyusiku tatu katika Madhabahu (Haram) Tukufu ya Hazrat Zainab (s.a).

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - Abna -, Sherehe / Hafla ya kuhuisha Mikesha ya nyusiku tatu za Lailatul-Qadr itafanywa na Bodi ya Wanazuoni wa Kiislamu wafuasi wa Shule ya Ahl al-Bayt (a.s) nchini Syria, katika Haram ya Hazrat Zainab (s.a). 

Hafla hii itafanywa kwa usimamizi wa Sheikh Ad'ham Khatib, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wanazuoni wa Kiislamu wa Skuli (Shule) ya Ahl al-Bayt (a.s) nchini Syria.

Marasimu (Hafla) hii ya kuhuisha nyusiku tatu za Lailatul-Qadr, itafanyika Machi (19, 21, na 23), 2025, sambamba na Usiku wa 19, 21, na 23 wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, kuanzia saa 21:00 kwa mujibu wa majira ya nchi husika. 

Ni huru kwa mabibi na mabwana, kaka na dada na watu wote kwa ujumla kuhudhuria katika hafla hii (kwa ajili ya kuungana kwa pamoja katika kuhuisha Masiku haya Matukufu ya Lailatul-Qadri).

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha