Maulamaa
-
Sheikh Naim Qassem:
Lebanon inapaswa kukabiliana kikamilifu na uvamizi wa kibeberu wa utawala wa Kizayuni | Mashahidi walijitolea kwa roho, mali na kila walichokuwa nacho
Lebanon inakabiliwa na uvamizi hatari wa Kizayuni: Akirejea mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel kusini mwa Lebanon, alisema: “Lebanon inakabiliwa na uvamizi wa hatari na wa kupanua mipaka wa utawala wa Kizayuni. Lazima tukabiliane nao kwa kila njia na mbinu. Adui huyu haheshimu makubaliano yoyote.”
-
Mkutano wa Kundi la Viongozi wa Kidini wa Kishia na Askofu Mkuu Mpya wa Washington
Kikundi cha viongozi wa kidini wa Kishia nchini Marekani pamoja na Askofu Mkuu wa Washington wamekutana katika kikao cha kirafiki ili kuimarisha ushirikiano kati ya Waislamu na Wakristo na kupanua njia za mazungumzo ya baina ya dini mbalimbali.
-
Maulid Kubwa Masjid Majmuuat - Temeke Mwisho Kufanyika Ijumaa Oktoba 17, 2025
Sheikh Dr.Alhad Mussa Salum amewahimiza Waumini wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani kuhudhuria kwa wingi, akisisitiza kuwa mwaka huu Maulid itakuwa na vionjo vya pekee, ikiwa ni kumbukumbu ya kumsifu na kufuata nyayo za Mtume Muhammad (s.a.w).
-
Salam za Rambirambi za Baraza la Maulamaa na Wenye Mamlaka wa Madhhebu ya Shia nchini Afghanistan Kufuatia Tetemeko la Ardhi Mashariki mwa Afghanistan
Baraza la Maulamaa na Watu Wenye Mamlaka wa Madhehebu ya Shia nchini Afghanistan, kupitia taarifa rasmi, limeeleza masikitiko na mshikamano wao na familia za waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni katika mkoa wa Kunar, mashariki mwa Afghanistan, huku likisisitiza umoja wa kitaifa na hitajio la msaada wa haraka kwa waathirika.