27 Aprili 2025 - 17:40
Hadithi / Tukio la  Kushusha Bendera ya Kuba ya Haram ya Bibi Zainab (a.s)

Imam wa Haram ya Bibi Zainab (a.s) alitangaza sababu ya kushushwa kwa bendera iliyokuwa juu ya Kuba ya Haram hiyo Tukufu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahluyll-Bayt (a.s) - ABNA - Vyanzo rasmi nchini Syria vilitangaza kuwa bendera iliyokuwa imeinuliwa juu ya Kuba ya Haram ya Bibi Zainab (a.s) ilishushwa.

Sheikh Ad'ham Khateeb, Imam wa Haram ya Bibi Zainab (a.s.) na Naibu Rais wa Baraza la Waislamu wa Shia la Syria, alielezea kuwa hatua hii ni ya muda na madhumuni yake ni kupita kipindi cha fitna. Alisisitiza kuwa Waislamu wa Syria hawatakubali kamwe kuwa na shinikizo lolote linalolazimishwa juu yao.

Aidha, alielezea kuwa bendera ya Kuba ya Haram ya Bibi Zainab (a.s), kama bendera nyingine zilizowekwa juu ya maeneo matakatifu ya Shia na Sunni, ina maana na alama maalum na haitoi matusi kwa kundi lolote au mtu yeyote.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha