24 Septemba 2025 - 06:56
Maulid Kubwa Masjid Majmuuat - Temeke Mwisho Kufanyika Ijumaa Oktoba 17, 2025

Sheikh Dr.Alhad Mussa Salum amewahimiza Waumini wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani kuhudhuria kwa wingi, akisisitiza kuwa mwaka huu Maulid itakuwa na vionjo vya pekee, ikiwa ni kumbukumbu ya kumsifu na kufuata nyayo za Mtume Muhammad (s.a.w).

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Imamu Mkuu wa Masjid Majmuuat Temeke Mwisho na Mwenyekiti wa Jumuia ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum al-Naqshbandi, ametangaza kuwa hafla kubwa ya Maulid ya Mtume (saww) jijini Dar es Salaam itafanyika Ijumaa, Oktoba 17, 2025 baada ya swala ya Isha katika viwanja vya msikiti huo.

Amesema maandalizi yako katika hatua za mwisho huku viongozi wa kitaifa wa Taasisi za Kiislamu, Maulamaa kutoka Zanzibar, Afrika Mashariki, pamoja na Masharifu na Masheikh kutoka Mikoa mbalimbali wakithibitisha kushiriki. Pia viongozi wa Serikali, Mabalozi, na viongozi wa vyama na taasisi za kiraia nao wamealikwa.

Sheikh Dr.Alhad Mussa Salum amewahimiza Waumini wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani kuhudhuria kwa wingi, akisisitiza kuwa mwaka huu Maulid itakuwa na vionjo vya pekee, ikiwa ni kumbukumbu ya kumsifu na kufuata nyayo za Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha