Maulid
-
Dar-es-Salam: Madrasah ya Hazrat Fatima Zahra (sa) Yaadhimisha Maulid ya Mtume Muhammad (saww)
Madrasah ya Hazrat Fatima Zahra (sa), iliyopo Wazo–Kinondoni, Dar es Salaam, imeandaa hafla maalumu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad Mustafa (saww), ikiwa na lengo la kuwakumbusha waumini na wanafunzi kuhusu mwenendo, maadili na mafundisho ya Mtume (saww).
-
Maulid ya Mtume Muhammad (saw) Yaadhimishwa katika Hawza Imam Ridha (as), Ikwiriri
Hafla ya kuadhimisha Maulid ya Mtume Muhammad Mustafa (saw) imefanyika katika Hawza Imam Ridha (as), Ikwiriri, Mkoa wa Pwani, ikishirikisha wanafunzi, walimu na waumini kutoka jamii ya Waislamu wa Shia na Sunni. Hotuba katika hafla hiyo imeangazia fadhila, tabia njema na mwenendo wa Mtume (saw), pamoja na upendo wake kwa watoto na umuhimu wa malezi bora ya kizazi kijacho.
-
Maulid ya Mtume Muhammad (saw) Yaadhimishwa kwa Pamoja na Waislamu wa Madhehebu Mbalimbali Mjini Moshi
Sherehe kubwa ya Maulid ya Mtume Muhammad (saw) imefanyika katika Madrasat Ummul-Banin (sa), mjini Moshi, Tanzania, kwa kushirikisha Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni. Hafla hiyo imekuwa jukwaa la kuimarisha upendo, undugu na umoja wa Kiislamu, pamoja na kueneza mafundisho ya Mtume (saw) na Ahlul-Bayt (as).
-
Waziri Mhe.Deus Sangu Akutana na Waislamu na Viongozi wa Kiislamu katika Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) Kigogo Post, Dar -es- Salaam
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Deus Sangu, ameshiriki katika hafla ya kumbukizi ya mazazi ya Mtume Muhammad (saww), iliyowakutanisha viongozi mbalimbali wa dini na serikali katika uwanja wa Kigogo Posti, Jijini Dar es Salaam.