Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Hafla kubwa ya Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) inatarajiwa kufanyika Ijumaa, tarehe 17 Oktoba 2025 baada ya Swala ya Isha, katika viwanja vya Masjid Majmuuat Al-Islaamiyyat - Temeke Mwisho, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Imamu Mkuu wa Msikiti huo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum Al_Shaadhiliy Al-Naqshabandiy Al-Dandaraqiy Al-Yushtutwiy, maandalizi yamekamilika kwa kiwango kikubwa na mahudhurio ya wageni mashuhuri yamepangwa vizuri.
Viongozi wa kitaifa wa taasisi za Kiislamu, Maulamaa kutoka Zanzibar, nchi za Afrika Mashariki, Masharifu na Masheikh wa Mikoa na Wilaya, pamoja na Viongozi wa Serikali, Mabalozi, vyama na taasisi za kiraia wote wamethibitisha kushiriki katika Maulid hii Tukufu ya Mtume Mtukufu - Muhammad (saww).
Dr. Alhad Mussa Salum ametoa wito kwa Waumini na watu wote wa Dar -es- Salaam na vitongoji vyake kuhudhuria kwa wingi katika hafla hiyo akisisitiza:
“Tumuadhimishe Mtume Muhammad (s.a.w.w), tumtukuze, na tufuate nyayo zake kwa upendo na amani.”
Hafla hii inatarajiwa kuwa miongoni mwa maadhimisho makubwa na yenye mvuto zaidi jijini Dar es Salaam mwaka huu.
Your Comment