Hafla
-
Sheikh Naeem Qassem:
"Kulenga Palestina, Muqawama na Iran ni sehemu ya vita moja / Mpango hatari wa Trump kwa Gaza: Vazi la Kimarekani juu ya mpango wa Kizayuni"
Katibu Mkuu wa Hizbullah nchini Lebanon, Sheikh Naeem Qassem, katika maadhimisho ya mwaka mmoja wa shahada ya mashujaa wawili wa muqawama — Shahid Sheikh Nabil Qawuq na Sayyid Suhail Al-Husseini — alionya kuhusu sura mpya ya mradi wa Kizayuni unaoitwa “Israel Kubwa” na kusisitiza juu ya kuendelea kwa mapambano na ulinzi wa mhimili wa haki.
-
Javier Bardem na Wasanii wa Hollywood Walaani Mauaji ya Kimbari ya Israel Katika ukanda wa Gaza - Wakiwa katika Hafla ya Tuzo za Emmy 2025
Javier Bardem, mwigizaji mashuhuri kutoka Hispania, katika hafla ya Tuzo za Emmy 2025 huko Los Angeles, alivutia hisia za hadhira kwa kuvaa kofia ya Kipalestina (kufiya) na kutamka kwa uwazi: "Nipo hapa kulaani mauaji ya kimbari yanayoendelea Gaza. Uhuru kwa Palestina!" Alieleza msimamo wake wa wazi na wa moja kwa moja dhidi ya ukatili wa Israel, na aliungwa mkono na wengi waliokuwepo ukumbini. Aidha, Bardem alitangaza kuwa anaunga mkono kampeni ya kususia kampuni na taasisi zinazoshirikiana na utawala wa Kizayuni (Israel), na akasambaza ujumbe wake wa mshikamano na Palestina kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Maana ya hatua yake: Kauli na kitendo cha Javier Bardem kinaashiria mshikamano wa wasanii kimataifa na watu wa Palestina, hasa katika nyakati ambapo jukwaa la burudani linaangaliwa na watu wengi duniani. Uvaaji wa chafia na kauli ya wazi ni ishara ya kuhamasisha umma wa kimataifa kushiriki katika harakati za kuunga mkono Palestina.
-
Rais wa Dar al-Iftaa ya Iraq asema:
“Ndio kwa Umoja wa Waislamu, ‘Hapana’ kwa Ubeberu wa Dunia”
Sheikh al-Sumayda‘i katika ufunguzi wa Mkutano wa Umoja alisema: "Lazima tuseme 'Ndio' kwa umoja wa Waislamu na, kwa kukataa ubeberu wa kimataifa, tuseme 'Hapana' kwa Magharibi na mabeberu."
-
China Yaonesha Nguvu za Kijeshi Katika Gwaride Huku Rais wa China Xi Akisimama Pamoja na Rais Putin na Rais Kim +Picha
China iliandaa gwaride kubwa la kijeshi kuonesha uwezo wake wa kivita, huku Rais Xi Jinping akisalimiana na kusimama pamoja na Rais Vladimir Putin wa Urusi na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un. Hafla hiyo iliangazia umoja wa kisiasa kati ya mataifa hayo na kuonesha silaha mpya na teknolojia ya kisasa ya kijeshi mbele ya maelfu ya watazamaji na viongozi wa kimataifa.
-
Wito kwa wananchi wa kushiriki kwa wingi kwenye mazishi ya Mashahidi wa Mamlaka ya ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Baraza la Uratibu wa Propaganda (Tablighi) za Kiislamu limetoa taarifa na kutangaza: Marasimu ya mazishi ya miili mitukufu ya mashahidi wa ngazi za juu kuwa itafanyika siku ya Jumamosi tarehe 27 Julai 2025, saa 8:00 Asubuhi mbele ya Chuo Kikuu cha Tehran.
-
Bilal Muslim Mission - Kanda ya Pangani - Hafla ya Mazazi ya Imam Ridha (as) na Maonyesho ya Wanafunzi wa Madrasa
Hafla hii imehudhuriwa na Madrasat kutoka Bilal Muslim – Kanda ya Pangani pamoja na baadhi ya Madrasa kutoka kwa ndugu zetu wa Kisuni. Hili ni jambo la faraja kubwa, linaloashiria mshikamano wa kijamii na wa kidini katika maeneo yetu.