25 Juni 2025 - 16:37
Wito kwa wananchi wa kushiriki kwa wingi kwenye mazishi ya Mashahidi wa Mamlaka ya ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Baraza la Uratibu wa Propaganda (Tablighi) za Kiislamu limetoa taarifa na kutangaza: Marasimu ya mazishi ya miili mitukufu ya mashahidi wa ngazi za juu kuwa itafanyika siku ya Jumamosi tarehe 27 Julai 2025, saa 8:00 Asubuhi mbele ya Chuo Kikuu cha Tehran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (as) -ABNA-, Baraza la Uratibu wa Propaganda za Kiislamu limetoa taarifa na kutangaza: Marasimu (Hafla) ya mazishi ya miili mitukufu ya mashahidi wa ngazi za juu katika jeshi na wanasayansi wa nyuklia, kuwa itafanyika Jumamosi, tarehe 27 Julai 2025, saa 8:00 Asubuhi mbele ya Chuo Kikuu cha Tehran.

Nakala ya tangazo hilo ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

إِنَّ الَّذِینَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَیْهِمُ الْمَلَائِکَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِی کُنْتُمْ تُوعَدُونَ (فصلت:۳۰ )

Wito kwa wananchi wa kushiriki kwa wingi kwenye mazishi ya Mashahidi wa Mamlaka ya ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Taifa adhimu la Iran ya Kiislamu, kufuatia hujuma na mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni katika ardhi takatifu ya Jamhuri ya Kiislamu, kundi la makamanda jasiri wa vikosi vya jeshi, wanasayansi mashuhuri wa nyuklia, na watu wasio na hatia, ambao ni pamoja na wanawake na watoto waliodhulumiwa, walifikia kiwango cha juu zaidi cha kifo cha kishahidi na imani. Kuchanganywa damu safi ya makundi mbalimbali ya watu na damu ya mashahidi wa nyuklia, maendeleo ya kisayansi na makamanda wa kijeshi waliojituma na kuwajibika kwa mamlaka na madaraka ya nchi ya Iran, kulikuwa na maana kubwa sana katika kudhihirisha uadui wa maadui dhidi ya maendeleo na mamlaka ya Iran.

Walinzi wa Mapinduzi wanautaarifu umma kwa ujumla kwamba shughuli ya mazishi ya miili mitakatifu ya mashahidi hao wa ngazi za juu itafanyika Jumamosi tarehe 27 Julai 2025, saa 8:00 Asubuhi mbele ya Chuo Kikuu cha Tehran. 

Baraza la Uratibu wa Propaganda za Kiislamu linawaalika wananchi wote wa taifa adhimu la Iran kuhudhuria hafla hii adhimu kwa shauku, ili kuhuisha dhamira yao kwa ajili ya itikadi za Mapinduzi ya Kiislamu na kuheshimu kumbukumbu za Mashahidi, na kwa mara nyingine kuonyesha azma yao thabiti ya kuilinda nchi hii, kusimama kidete na kukabiliana na maadui, na kudhihirisha sapoti na uungaji wao mkono wa pande zote dhidi ya utawala muovu na wa jinai wa Kizayuni na Marekani.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha