Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Sheikh Khalifa Khamis, Mwanachuoni maarufu wa Kisunni nchini Tanzania, amesema kuwa nafasi ya Iran katika siasa za kimataifa imeifanya dunia kuitambua kama taifa kubwa lenye nguvu na ushawishi mkubwa katika masuala ya kikanda na kimataifa.
Akizungumzia matukio mbalimbali yanayoendelea katika ulimwengu wa Kiislamu na kimataifa, Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa dunia ya leo imefikia hatua ya kukiri nafasi muhimu ya Iran katika medani ya siasa za dunia na maendeleo ya ulimwengu wa Kiislamu.

Katika mada maalumu kuhusu Iran, Sheikh Khalifa Khamis pia alimuenzi Ruhollah Khomeini kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha hadhi ya Uislamu na Waislamu duniani. Mada hiyo ilibeba anuani isemayo: "Imam Khomeini Aliupa Nguvu Uislamu Kidini, Kisiasa na Kijeshi."
Kwa mujibu wa Sheikh Khalifa, mchango wa Imam Khomeini (ra) haukuishia katika kuongoza Iranian Revolution pekee, bali ulihusisha pia kuimarisha utambulisho wa Kiislamu, kujitegemea kisiasa na kujenga uwezo wa kujilinda dhidi ya vitisho vya nje.
Ameongeza kuwa athari za fikra, maono na harakati za Imam Khomeini (ra) zinaendelea kuonekana hadi leo, huku Iran ikiendelea kuwa miongoni mwa mataifa yenye ushawishi mkubwa katika masuala ya ulimwengu wa Kiislamu na siasa za kimataifa.
Your Comment