Imam Khomeini (RA)
-
Sheikh Isa Qassim: Kiongozi Shahidi alisimama kwa ajili ya Uislamu, Umma na ubinadamu
Mwanazuoni mashuhuri wa Bahrain, Ayatullah Sheikh Isa Ahmad Qassim, amesema kuwa Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alijitolea maisha yake kwa ajili ya Uislamu, Umma wa Kiislamu na ubinadamu, huku akieleza kuwa urithi wake utaendelea kuongoza njia ya Muqawama na umoja wa Waislamu.
-
-
Sheikh Khalifa Khamis: Dunia Sasa Yakiri Iran ni Taifa Kuu
Sheikh Khalifa Khamis amesema dunia sasa imeitambua Iran kama taifa kubwa, akisisitiza kuwa Imam Khomeini (ra) aliupa Uislamu nguvu katika nyanja za kidini, kisiasa na kijeshi.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Kumtambua Imam Khomeini ni Taa ya Kuongoza Mustakabali wa Iran
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Seyyed Mojtaba Khamenei, amesema kuwa kuelewa na kumtambua Ruhollah Khomeini ni mwanga unaoongoza mustakabali wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Amebainisha kuwa kufuata mwenendo wa Ali ibn Abi Talib kumekuwa alama ya fahari kwa viongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, huku akisisitiza kwamba taifa la Iran limesimama bega kwa bega na Muqawama na kuwa mfano wa kujivunia kwa mataifa yanayotafuta uhuru. Aidha, amewataka wananchi kudumisha umoja, busara na kuaminiana ili kuvuruga njama za maadui na kulinda mafanikio ya Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s): Imam Khomeini (r.a) Aliirejesha Dini Kutoka Pembezoni Hadi Kiini cha Jamii na Utawala
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s), Ayatullah Reza Ramadhani, amesema kuwa Imam Khomeini (r.a) aliirejesha dini kutoka pembezoni hadi kuwa kiini cha maisha ya kijamii na mfumo wa utawala, akithibitisha kuwa dini inaweza kuwa msingi wa uongozi, haki ya kijamii na ujenzi wa ustaarabu wa kisasa.
-
Irani Dhidi ya Magharibi: Kutoka Uzoefu wa Kihistoria Hadi Mapambano ya Kistaarabu ya Leo
Mkutano “Sisi na Magharibi katika Mitazamo na Fikra za Ayatullah Al-Udhma Sayyid Ali Khamenei” wafanyika Tehran.
-
Sayyid Ali Khomeini: “Kama Ubalozi wa Marekani usingelivamiwa, leo tusingekuwa na Makombora wala ishati ya nyuklia"
Akiisisitizia kauli kwamba “uvamizi wa ubalozi wa Marekani uliimarisha uhuru wa Iran,” alisema: “Kama tukio hilo lisingetokea, leo hii Jamhuri ya Kiislamu isingekuwepo, na nchi yetu isingepata teknolojia ya makombora na nishati ya nyuklia, kwani Marekani ilikuwa inapinga maendeleo haya.”
-
Nafasi ya Marājiʿ wa Kishia katika Kulinda Umoja wa Ardhi na Utambulisho wa Kitaifa- Sehemu ya 2 | Marāji ni, Walinzi wa Uhuru wa Nchi za Kiislamu
Mfano mashuhuri ni Ayatullah al-Uzma Sayyid Muhammad Hasan Shirazi, ambaye alitoa Fat'wa maarufu ya kupiga marufuku tumbaku mwaka 1891 huko Iran, hatua iliyozuia njama za kikoloni za Waingereza na kuwa alama ya mapambano ya Kiislamu dhidi ya ukoloni. Vivyo hivyo, Ayatullah Kashif al-Ghita, Ayatullah Muhsin al-Hakim, na Imam Khomeini (r.a) walikuwa mstari wa mbele katika kuhimiza mapambano ya kulinda utu, uhuru, na heshima ya mataifa ya Kiislamu.
-
Ayatullah Malakooti:
"ABNA Ina Wajibu wa Kutambulisha Madhehebu ya Ahlul-Bayt (A.S) Ulimwenguni / Baba Marehemu alikuwa wa Awali Kusaini kuondolewa kwa Shah"
Akizungumza na Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (ABNA) Jumapili, 20 Mehr 1404 (2025), Ayatullah Malakooti alisisitiza umuhimu wa kueleza Ushia kwa usahihi mbele ya upotoshaji. Alieleza kuwa kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu, dunia haikuufahamu Ushia kama ilivyostahili; taarifa nyingi zilizokuwepo zilitokana na maandiko ya Ahlus-Sunnah yaliyo na taarifa zisizokamilika au kwa makusudi kutoeleza Ushia kwa usahihi, na hivyo Ushia / Mashia walichukuliwa kama kundi dogo au la upande mmoja.
-
Mpango wa Kubadilisha Paradigm ya Mapinduzi ya Kiislamu; Mbinu ya Ubeberu wa Dunia kwa Ajili ya Kutawala Taifa la Iran
Kikao cha kitaalamu chenye mada ya “Ukosoaji na Uchambuzi wa Mpango wa Kubadilisha Paradigm katika Mapinduzi ya Kiislamu; maana na sababu zake kwa mujibu wa fikra za Imam Khomeini (r.a) na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu” kimefanyika kwa juhudi za Idara Kuu ya Utafiti wa Kiislamu ya Shirika la Utangazaji la Taifa.
-
Dkt. Pezeshkian: Umoja na Mshikamano Nguvu Yetu Dhidi ya Maadui
Alionya dhidi ya kuvunjika kwa mshikamano wa taifa na urafiki wa majirani, akibainisha kuwa hayo ni malengo ya Marekani na Israel ya kuleta mgawanyiko miongoni mwa Waislamu na nchi za jirani.