Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Imam Khomein (rehmatullah alayh) yamefanyika katika Chuo cha Jamiat Al-Mustafa (s) kilichopo Dar es Salaam, Tanzania, na kuhudhuriwa na mamia ya watu, wakiwemo viongozi mbalimbali wa kidini na kisiasa, akiwemo Mheshimiwa Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania.
Imam Khomein (ra) alikuwa kiongozi wa kipekee aliyesimama kidete kutetea Uislamu katika vipindi vyote vya maisha yake. Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, alifanikiwa kuasisi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambayo hadi leo inaendelea kuwa mfano wa kuigwa na mataifa mengi duniani, kutokana na mafanikio yake katika nyanja mbalimbali kama vile kijeshi, kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Imam Khomein (ra) anakumbukwa duniani kote kama mtetezi wa wanyonge, hususan kwa msimamo wake thabiti katika kuwatetea Waislamu wa Palestina na wananchi wa Palestina kwa ujumla.
Your Comment