Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA -; Jopo la Wanawake la Kongamano la 6 la Kimataifa la Quds Tukufu lenye jina la "Tuelekee Al-Quds" litafanyika kwa kuhudhuriwa na masista (wadada) mahiri kutoka nchi mbalimbali.
Mada za mkutano huu zitakazowasilishwa na Wataalam (Wachambuzi) ni hizi zifuatazo:
1. Imam Khomeini (RA) na utoaji wa mfano wa mahudhurio ya Wanawake wenye kujitolea katika nyanja tofauti za jamii.
2. Utandawazi wa mtindo wa Upinzani (Muqawamah) wa Wanawake wa Kiislamu kwa kuhimizwa na Hazrat Zainab (s.a).
3. Masimulizi ya vipimo vya Wanawake wa Kiislamu wa Kipalestina katika kufichua dhulma na ukatili wa adui Mzayuni.
4. Matumaini, motisha na roho ya kishujaa ya Upinzani (Muqawamah) wa Wanawake na nafasi yake katika kuleta ushindi.
5. Nguvu na kutochoka katika Mapambano ya Wanawake wa Kiislamu (Phoenix inaongezeka).
Tanbihi: Unapoelezea kitu au mtu kuwa mtu huyu ni "Phoenix", unamaanisha kwamba mtu huyo ananarudi tena (na anainuka tena) upya baada ya kuonekana kutoweka au kupotea au kusambaratishwa.
Mkutano huu utafanyika Jumanne, Machi 25, 2025, kuanzia saa 16:00 PM hadi adhana ya Maghrib, Jijini Tehran, barabara ya Keshavarz, mbele ya Park ya Laleh, kabla ya kufika katika mtaa wa Quds No. 228, katika jengo la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS).
Wale wenye nia na wanaotaka kufuatilia Kongamano hili, wanaweza kufuatilia na kutazama kangamano hilo kupitia matangazo ya moja kwa moja ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna -.
Your Comment