Kongamano
-
Uzinduzi wa Wito wa Kongamano la Kimataifa la “Umana'u al-Rusul”;
Kusisitizwa Nafasi ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah katika Umoja na Muqawama wa Kiislamu
Hafla ya uzinduzi wa bango la mwito wa kuwasilisha makala kwa Kongamano la Kimataifa la “Umana'u al-Rusul”, lenye kaulimbiu “Umoja na Muqawama wa Kiislamu katika Fikra za Shahidi Nasrallah, kwa kuzingatia uwezo wa kimkakati wa Mkoa wa Hormozgan,” imefanyika. Katika hafla hiyo, wazungumzaji walieleza kwa kina vipengele mbalimbali vya haiba ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, fikra zake, mwenendo wake wa kijihadi, pamoja na nafasi yake katika kuimarisha umoja wa Kiislamu na harakati ya Muqawama.
-
Kitabu cha “Hakimu wa Umma” chazinduliwa Kargil, India
Taasisi ya Utafiti na Elimu ya Baqir al-Ulum (as) ya Kargil, India, imeandaa mkutano wa kielimu na kifasihi wenye kaulimbiu “Sauti ya Zainab (sa)”, uliowakutanisha wanazuoni, wasomi, washairi, wanafunzi wa vyuo vya dini na vyuo vikuu. Katika hafla hiyo, kitabu “Hakimu wa Umma” kimezinduliwa, huku washindi wa mashindano ya usomaji wa vitabu kwa vijana wakitunukiwa.
-
Nablus Yapokea Kongamano na Kikao cha Kumuenzi Kiongozi wa Iran
Kongamano na kikao cha kumbukumbu kilifanyika katika mji wa Nablus, Ukingo wa Magharibi, kwa ushiriki wa wanaharakati wa utamaduni na vyombo vya habari, ambapo washiriki walijadili mchango wa Kiongozi wa Iran katika siasa za kikanda na msimamo kuhusu Palestina.
-
Kitabu cha Mwanazuoni Mkristo Kuhusu Imam Hussein (as) Chazinduliwa Karbala
Kongamano la kimataifa la "Imam Hussein (as) kwa Mtazamo wa Dini na Madhehebu" limefanyika Karbala, ambapo kitabu kipya cha Profesa Chris Hewer, mwanazuoni Mkristo kutoka Uingereza, kilizinduliwa huku washiriki wakisisitiza kuwa ujumbe wa Ashura ni wa wanadamu wote.
-
Watafiti waalikwa kuwasilisha tafiti katika Kongamano la Pili la Kimataifa la Ustaarabu wa Kiirani na Kiislamu litakalofanyika Vienna
Kongamano la Pili la Kimataifa la Ustaarabu wa Kiirani na Kiislamu limetoa wito kwa wasomi, watafiti na wanafunzi wa shahada za juu kutoka duniani kote kuwasilisha tafiti zao, huku mada kuu ikiwa ni nafasi ya wanawake katika ustaarabu wa Kiirani tangu zama za kale hadi leo.
-
Katika kikao na waandaaji wa kongamano la Mirza Naeini,
Kiongozi wa Mapinduzi amesema: Ubunifu wa kielimu na fikra za kisiasa ndizo sifa mbili mashuhuri za Allamah Naeini
Matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alipokutana na washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Allamah Mirza Na'ini yamechapishwa leo asubuhi katika ukumbi wa mkutano huo mjini Qom.