Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul Bayt (a.s) – ABNA – Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa "Waandishi wa Habari wa Ahlul Bayt (a.s)" umeanza leo hii asubuhi katika Mji wa Qom, ikiwa ni sambamba na Mnasaba wa maadhimisho ya "Siku Kumi (10) zenye Baraka" / عشرة أيام المباركة kwa ushiriki wa Wanahabari na Wasomi kutoka Iran na Bara la Afrika. Tukio hili limeandaliwa na Shirika la Kimataifa la Habari la Ahlul Bayt (a.s) – ABNA – Katika ukumbi wa mikutano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s).
Hafla hii ya vyombo vya habari imeambatana na hotuba kutoka kwa Ayatollah Reza Ramezani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bayt (a.s), na Dkt. Sayyid Mohammadamin Aghamiri, Mjumbe wa Baraza Kuu la Mtandao na Mkuu wa Kituo cha Kitaifa cha Mtandao nchini Iran. Pia kulikuwa na ujumbe wa video kutoka kwa Hojjatul Islam wal Muslimin Sheikh Ibrahim Zakzaky kuhusiana na tukio hili la la Vyombo vya Habari na Wanaharakati wa Habari wa Ahlul-Bayt (a.s) katika mitandao mbalimbali ya Kijamii. Sheikh Ibrahim Zakzaky amewapongeza washiriki katika Kongamano hili la wanahabari wa Ahlul-Bayt (a.s) na kuongelea zaidi umuhimu wa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii katika kueneza maarifa sahihi ya Uislamu kwa mujibu ya Muongozo wa Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wake watoharifu (a.s).
Katika hafla hiyo, wawakilishi walioteuliwa kutoka kwa Wanahabari wa Bara la Afrika wametoa maoni na mitazamo yao mbalimbali kuhusiana na suala la vyombo vya habari na mitandao ya kijamii katika kueneza mafunzo matukufu ya Kiislamu.
Aidha, kumezinduliwa toleo jipya la Shirika la Habari la ABNA katika lugha 27.
Mwisho, washiriki wameppata fursa ya kushiriki katika zoezi la kupiga kura ili kuchagua Wanahabari 14 wa Ahlul-Bayt (a.s) kutoka katika Bara la Afrika ambao watapatiwa tiketi na kila kinachohitaji kwa ajili ya kwenda katika Mji Mtukufu wa Mash-Had kumzuru Imam Ridha (a.s), Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Your Comment