Muqawamah
-
Nyuma ya Pazia la Uhalifu wa Vyombo vya Habari: Kumvunjia heshima Sayyid wa Mashahidi wa Muqawama kupitia Kituo kimoja cha Televisheni cha Kilebanon
Hivi karibuni, televisheni ya Al-Jadeed ilirusha ripoti kutoka kwenye Kaburi la Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, ambapo ilitoa matamshi ya matusi dhidi ya shahidi huyu wa umma. Tukio hilo liliwaudhi sana wananchi wa Lebanon na kuumiza hisia zao. Mbunge mmoja wa Lebanon alitoa onyo kali kuhusu uhalifu huu wa vyombo vya habari na athari zake kwa umoja wa kitaifa.
-
Mashambulizi ya makombora ya Muqawama wa Palestina katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu
Vyanzo vya habari vimeripoti shambulio la roketi kutoka Ukanda wa Gaza kwenye maeneo yanayokaliwa kimabavu ya Palestina.
-
Jumuiya ya walimu wa Seminari ya Qom:
Wananchi wa Iran wanapaswa kutangaza utayarifu wao wa kuwasaidia wapiganaji wa Palestina kwa kushiriki katika maandamano ya Siku ya Quds
Katika kizingiti cha Siku ya Quds Duniani, Jumuiya ya Walimu wa Seminari ya Qom imetoa taarifa ikizitaka sehemu zote za Taifa pendwa la Iran kushiriki kikamilifu katika Matembezi ya Amani ya Siku hii ya Quds na kutangaza kwa mara nyingine uungaji mkono wao kwa Muqawamah (Upinzani) wa Kiislamu wa Palestina.
-
Jopo la Wanawake la Kongamano la 6 la Kimataifa la Quds Tukufu litafanyika
Kongamano hili lenye jina la "Tuelekee Al-Quds" litafanyika siku ya Jumanne, tarehe 25 Machi, 20205 Jijini Tehran, katika jengo la Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (AS).