31 Agosti 2025 - 17:39
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Lalaani Mauaji ya Kinyama ya Wazayuni Dhidi ya Yemen-Laahidi Jibu Kali kutoka kwa Muqawama wa Kiislam

"Kinyume na matarajio ya Wazayuni na waungaji mkono wao, jinai hizi hazitaweza kudhoofisha irada ya mapambano ya wananchi wa Yemen, bali damu ya mashahidi hawa watukufu itachochea zaidi hasira na mwamko wa upinzani dhidi ya ukoloni na utawala wa Kizayuni kote katika eneo".

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Tehran - Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limetoa tamko kali kulaani shambulio la kikatili lililofanywa na utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya watu wa Yemen, ambalo limesababisha kuuawa shahidi kwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Mabadiliko na Ujenzi ya Yemen, Ahmed Ghalib Nasser al-Rahwi, pamoja na mawaziri wengine na wafuasi wao.

Katika taarifa hiyo rasmi, IRGC limeeleza kuwa shambulio hilo ni mfano wazi wa ugaidi wa kiserikali na jinai dhidi ya ubinadamu, na limedhihirisha tena uso halisi wa utawala wa Kizayuni kuwa wa kinyama, wa kibaguzi, na wa kiudhalimu.

Sehemu ya Taarifa ya IRGC:

"Kinyume na matarajio ya Wazayuni na waungaji mkono wao, jinai hizi hazitaweza kudhoofisha irada ya mapambano ya wananchi wa Yemen, bali damu ya mashahidi hawa watukufu itachochea zaidi hasira na mwamko wa upinzani dhidi ya ukoloni na utawala wa Kizayuni kote katika eneo."

IRGC imeongeza kuwa utawala wa Kizayuni unalindwa moja kwa moja na Marekani, huku taasisi nyingi za kimataifa zikibaki kimya mbele ya uhalifu wake. Jinai hizi zinaleta tishio kubwa kwa usalama wa eneo na dunia nzima.

Jeshi hilo limebainisha kuwa:

"Muqawama wa Kiislamu katika eneo, likiwemo taifa jasiri la Yemen, litatoa jibu kali, la kuadhibu na la kutisha dhidi ya wauaji Wazayuni."

"Tunaziomba serikali zote za Kiislamu, mashirika ya haki za binadamu na taasisi za kimataifa kuacha ukimya na kuchukua hatua za wazi, madhubuti na za kivitendo ili kukomesha jinai hizi."

Katika hitimisho lake, IRGC limeeleza kusimama imara pamoja na mataifa ya Palestina na Yemen na kuahidi kuendeleza kila juhudi ya kupambana na uvamizi na dhulma, hadi haki ipate ushindi na utawala wa kinyonyaji ushindwe.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha