29 Septemba 2025 - 14:35
Rais wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan: Shahada ya Sayyid Hassan Nasrallah Imeongeza Msaada wa Kijamii kwa Hizbullah

Rais wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, alisema: Shahidi Hassan Nasrallah alikuwa mjahid mkubwa katika zama zake, na kwa shahada yake msaada na uungaji mkono wa kijamii kwa Hizbullah umeongezeka.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la AhlulBayt (a.s) -ABNA- Ayatollah Sayyid Sajid Ali Naqvi, Rais wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan, katika kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, alibainisha kuwa: Shahidi Hassan Nasrallah alikuwa mjahid mkubwa katika zama zake, na shahada yake imeongeza msaada na nguvu ya kijamii kwa Hizbullah.

Aliongeza: Harakati ya ukombozi wa Baytul-Maqdis na vuguvugu za muqawamah wa Kiislamu vimeimarika, na matokeo yake nguvu za kibeberu zimekumbwa na fedheha na kushindwa.

Ayatollah Naqvi alisisitiza: Shahada na kujitolea kwa namna ya kipekee kwa shahidi huyu kumejenga nafasi ya pekee katika kiwango cha kimataifa na kumesababisha mabadiliko makubwa duniani kote, hususan katika eneo hili.

Rais wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan aliendelea kueleza: Hali ya sasa ni mbaya sana na ukweli wa uwanjani unaonyesha kuwa chanzo cha uharibifu huu ni nguvu za kibeberu. Utawala wa Kizayuni, ukiwa na rasilimali zote, bajeti, silaha za kisasa, teknolojia, taarifa na mipango, unafanya kazi chini ya usaidizi na uangalizi wa nguvu za kibeberu. Kupitia msaada huu, utawala huo haramu kwa miaka miwili sasa umeendeleza uharibifu na mauaji huko Gaza na pia Lebanon. Katika hali hii, jamii ya kibinadamu inapaswa kujitahidi kudhibiti unyama na jinai hizi.

Akaendelea kusema: Pakistan ina uwezo na ushawishi wa kutosha ambao kwa diplomasia thabiti na upigaji debe wa kimkakati inaweza kuongeza shinikizo kwa nguvu za kibeberu ili kumaliza uvamizi na ukatili huko Gaza, Palestina na Lebanon, na hata kuzuia kutokea kwa Vita Kuu ya Tatu ya Dunia.

Ayatollah Naqvi pia alisisitiza umuhimu wa kuimarisha misaada ya kibinadamu kwa watu wanyonge wa Gaza, Palestina na Lebanon.

Mwisho, akiheshimu kujitolea kwa shahidi Sayyid Hassan Nasrallah na wenzake, aliomba Dua kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu awape mujahidina wa Hizbullah tawfiki na ujasiri wa kuendeleza njia hadi kufanikisha jukumu lao.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha