Rais wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan amesema kuwa:
Uislamu ni mfumo kamili wa maisha ambao ni mtangulizi wa haki sawa, uadilifu wa kiuchumi na utawala wa haki, na mfano bora zaidi wa hayo ni mfumo wa haki wa Imam Ali (a.s) ambao utabaki kuwa kielelezo cha uadilifu na usawa daima.
Rais wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, alisema: Shahidi Hassan Nasrallah alikuwa mjahid mkubwa katika zama zake, na kwa shahada yake msaada na uungaji mkono wa kijamii kwa Hizbullah umeongezeka.