Sayyid Hassan Nasrallah
-
Marasimu adhimu ya “Siku ya Shahidi” yafanyika Beirut
Sheikh Naeem Qassem: “Siku ya Shahidi si tu kwa ajili ya kuwakumbuka mashahidi, bali pia ni heshima kwa familia zao na wote wanaounga mkono njia ya mapambano ya muqawama.”
-
Ripoti ya ABNA kutoka katika hafla ya kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuuawa kishahidi kwa watangulizi wa mhimili wa mapambano, huko Qom;
"Nasrallah hakuwa mtu, bali alikuwa ni shule ya fikra / Silaha ya mapambano itaendelea kubaki" + Picha na Video
Hujjatul-Islam Naser Rafii, katika hafla ya kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kuuawa kishahidi kwa watangulizi wa mhimili wa mapambano, alisema: "Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa mbebaji bendera ya mapambano na kielelezo cha shule ya fikra, na njia yake itaendelea."
-
Profesa kutoka Lebanon katika mahojiano na ABNA:
Jina la Nasrallah limehusishwa na usalama na uaminifu / Silaha za Hezbollah zitaendelea kuwa sehemu ya mlingano wa Lebanon na eneo la kikanda
Yeye (Sayyid Hassan Nasrallah) alihesabiwa kuwa alama ya heshima na mapambano kwa wote, na alikuwa mfano wa malengo ya sehemu kubwa ya wapiganaji wa muqawama wa Kishia ambao kwa vitendo walitaka kufikia mamlaka, uhuru, na kujitegemea kwa Lebanon.
-
Rais wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan: Shahada ya Sayyid Hassan Nasrallah Imeongeza Msaada wa Kijamii kwa Hizbullah
Rais wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, alisema: Shahidi Hassan Nasrallah alikuwa mjahid mkubwa katika zama zake, na kwa shahada yake msaada na uungaji mkono wa kijamii kwa Hizbullah umeongezeka.
-
Mkutano wa Wanafunzi wanaoongea Lugha ya Kiurdu Wanaokaa Mjini Qom - Iran; katika Kumbukumbu ya Mwaka wa Shahada ya Sayyid Hassan Nasrallah
Hujjatul-Islam Fakhrian aliandika mada yake kwa kuanzia na nukuu ya Kiungu (alirejea aya za Quran) na kutangaza kuwa: azma ya Mwenyezi Mungu ni kuwapa walio dhaifu nafasi ya kuwa waanzilishi na warithi wa dunia; azma hiyo inatimia kwa njia moja tu — kupitia mapambano na kujitolea. Kwa hivyo, alisisitiza, hakuna njia nyingine ya kuangusha mfumo wa udikteta wa kigeni isipokuwa kupitia mapambano.
-
Sheikh Naeim Qassem: „Kwa mapigano ya aina ya Karbala, tutakabiliana na kuondolewa kwa silaha za harakati ya upinzani.“
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, katika hotuba ya kumbukumbu ya mashahidi Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim Safiuddin, amesisitiza kuwa Hizbullah imesalia thabiti katika ahadi yake na itapinga vikali jaribio lolote la kuondoa silaha zake.
-
Shahidi Sayed Hasan Nasrallah kwa maneno ya binti yake wa pekee
Kituo cha habari “Asr” kimechapisha mahojiano ya kwanza ya kipekee na Zainab Nasrallah, binti wa pekee wa shahidi Sayed Hasan Nasrallah.
-
Katika mazungumzo na ABNA:
Ushuhuda wa Dada wa Shahidi Abbas Mousavi Kuhusu Kiongozi wa Muqawama:Syed alikuwa Mpenzi wa Mungu -Tulipata nguvu na matumaini kutoka kwa hotuba zake
Bi Hoda Mousavi, dada wa shahidi Sayed Abbas Mousavi, Katibu Mkuu wa zamani wa Hezbollah Lebanon, amesema: Sisi daima tulihisi katika maneno na mwongozo wake kwamba yeye kwanza kabisa alikuwa mpenzi wa Mungu. Mara tu tuliposikiliza hotuba zake, tulivutiwa kimagnet kwa hisia kwake; siri ya hilo ilikuwa katika ikhlasi na uaminifu wake kwa mpenzi wake wa kimungu.
-
Majlisi ya Kumbukumbu ya Shahada ya Sayyid Hassan Nasrallah Kufanyika Beirut
Katika hafla hiyo: Mzungumzaji mkuu atakuwa Sheikh Muhammad Sadiq.
-
Mtazamo juu ya Septemba ya Umwagaji Damu Lebanon;Kuanzia Jinai za Pagers hadi Subira ya Kistratejia ya Hizbullah baada ya Shahidi “Sayyid wa Muqawama"
Siku hizi ni kumbukumbu ya jinai za kipekee za utawala wa Kizayuni nchini Lebanon – kuanzia milipuko ya pageri hadi mauaji ya makamanda waandamizi wa Hizbullah. Hivyo basi, Septemba ya mwaka uliopita kwa Wana-Lebanon imekuwa mwezi usiosahaulika
-
Kuuawa Kishahidi kwa Abu Ali,Mkuu wa timu ya Ulinzi wa Shahidi Nasrullah, pamoja na «Sayyid Haidar Al-Muwa'li» Naibu wa Kataib Sayyid AlShuhadaa, Iraq
"Kwa Masikitiko, tumepata habari kuwa mmoja wa makamanda wa Kataib Sayyid al_Shuhada, Sayyid Haidar Al-Muwa'li, Naibu wa Abu A'la'i Al-Wila'yi, Katibu Mkuu wa Kataib Sayyid al-Shuhada, amepata kifo cha Kishahidi wakati wa shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran."
-
Nyuma ya Pazia la Uhalifu wa Vyombo vya Habari: Kumvunjia heshima Sayyid wa Mashahidi wa Muqawama kupitia Kituo kimoja cha Televisheni cha Kilebanon
Hivi karibuni, televisheni ya Al-Jadeed ilirusha ripoti kutoka kwenye Kaburi la Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, ambapo ilitoa matamshi ya matusi dhidi ya shahidi huyu wa umma. Tukio hilo liliwaudhi sana wananchi wa Lebanon na kuumiza hisia zao. Mbunge mmoja wa Lebanon alitoa onyo kali kuhusu uhalifu huu wa vyombo vya habari na athari zake kwa umoja wa kitaifa.
-
Kuchapishwa kwa kitabu cha kwanza kuhusu Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah kwa ajili ya Watoto
Kitabu cha kwanza cha Watoto na Vijana kuhusu Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, kilichoitwa "Baba Hadi" kilichoandikwa na: Elaheh Akherati, kimechapishwa na sasa kinapatikana kwa wale wanaotaka.