15 Septemba 2025 - 12:21
Mtazamo juu ya Septemba ya Umwagaji Damu Lebanon;Kuanzia Jinai za Pagers hadi Subira ya Kistratejia ya Hizbullah baada ya Shahidi “Sayyid wa Muqawama"

Siku hizi ni kumbukumbu ya jinai za kipekee za utawala wa Kizayuni nchini Lebanon – kuanzia milipuko ya pageri hadi mauaji ya makamanda waandamizi wa Hizbullah. Hivyo basi, Septemba ya mwaka uliopita kwa Wana-Lebanon imekuwa mwezi usiosahaulika

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa AhlulBayt (a.s) -ABNA- Hizbullah ya Lebanon tangu mwanzo wa Operesheni “Tofaan al-Aqsa” iliingia vitani kwa lengo la kutetea wananchi wanyonge wa Gaza na kulinda usalama na umoja wa ardhi ya Lebanon, ikiwa kama ngome kuu ya kusaidia Gaza. Kila siku Hizbullah ilifanya makumi ya mashambulizi dhidi ya kaskazini mwa ardhi za Palestina zilizokaliwa kwa mabavu, kiasi kwamba maeneo ya kijeshi ya Israel yalibaki tupu.

Historia ya uhai haramu wa utawala wa Kizayuni imejaa misururu ya mauaji ya kigaidi kila mara unaposhindwa vitani. Katika muktadha huo, ili kukabiliana na mapigo makali ya Hizbullah, kikosi cha mauaji cha Israel kilianzisha jinai kubwa dhidi ya wananchi na viongozi wa Lebanon.

Milipuko ya pageri iliyoratibiwa kwa siku mbili mfululizo ilisababisha majeraha na mashahidi kwa maelfu ya Wana-Lebanon.

Marehemu Seyyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa zamani wa Hizbullah, baada ya jinai hiyo alisema:

“Adui siku ya Jumanne alilenga pageri 4,000. Kisha siku iliyofuata akalipua tena pageri kwa shabaha ya kuua watu 5,000. Mauaji haya ni jinai ya kivita na ni tangazo la vita dhidi ya Lebanon.”

Mtazamo juu ya Septemba ya Umwagaji Damu Lebanon;Kuanzia Jinai za Pagers hadi Subira ya Kistratejia ya Hizbullah baada ya Shahidi “Sayyid wa Muqawama"

Mauaji ya Viongozi na Shahada ya Sayyid wa Muqawama

Mauaji mfululizo ya makamanda wa muqawama na hatimaye kuuawa shahidi kwa Katibu Mkuu wa Hizbullah yalikuwa pigo kubwa zaidi kwa mwili wa muqawama nchini Lebanon. Hata hivyo, baada ya mwaka mmoja kupita, licha ya shinikizo la Marekani na nchi za Magharibi kutaka kuunda serikali inayolenga kuibadilisha au kuibana Hizbullah, muqawama bado umesimama imara ukiendeleza njia yake kwa subira ya kistratejia.

Mwandishi wa habari Zulfiqar Daher katika al-Manar aliandika:
“Septemba ya mwaka huu ilikuwa nzito, ikiakisi maumivu na fidia kubwa ya mwaka uliopita, ambapo viongozi wakubwa wakiongozwa na Seyyid Hassan Nasrallah – Seyyid wa mashahidi wa Umma – pamoja na ndugu na makamanda walithibitisha hadhi na uwezo wa muqawama.”

Mashambulizi hayo yalilenga hasa kusini, Bekaa na Dahieh ya kusini mwa Beirut, bila kuacha mji mkuu na maeneo ya kaskazini na Jabal Lebanon.

Umuhimu wa Mlingano wa “Jeshi -Muqawama- Umma”

Pamoja na fidia zote, wananchi na muqawama walionyesha uimara wa ajabu wa kihistoria unaohitaji utafiti na uchambuzi wa kina kwa ajili ya kuelewa sababu, mazingira na athari zake. Matokeo yake sio tu katika kudumu kwa muqawama, bali pia katika mlingano wa kisiasa wa kanda nzima, hususan mustakabali wa uwepo wa Israel, ambayo licha ya uhalifu wake haikuweza kuuangamiza muqawama.

Katika tukio la kihistoria, tarehe 27 Septemba 2024 – kuuawa shahidi kwa Seyyid Hassan Nasrallah – ulikuwa ni upeo wa pekee. Aidha kumbukumbu ya tarehe 12 Septemba 1997 – shahada ya mwanawe Hadi Nasrallah katika vita vya Jabal al-Rafi – imebaki kama alama angavu ya familia ya muqawama na ya Seyyid Nasrallah binafsi.

Mtazamo juu ya Septemba ya Umwagaji Damu Lebanon;Kuanzia Jinai za Pagers hadi Subira ya Kistratejia ya Hizbullah baada ya Shahidi “Sayyid wa Muqawama"

Kauli za Wataalamu

Dk. Ali Hamiyah, mtaalamu wa masuala ya kistratejia, alisema:
“Kadiri muqawama unavyokabiliwa na shinikizo, ndivyo unavyokuwa na nguvu zaidi. Muqawama unakua tu ukiwa umepungiwa. Haukuanguka mbele ya adui wa Kizayuni wala mbele ya meli na vikosi vya Magharibi. Leo bado tunaweza kusimama na hakika tutashinda.”

Aliendelea:
“Septemba 2024 ilikuwa ya kutikisa, makamanda waliuawa shahidi, lakini muqawama uliendelea kupigana na ukashinda. Bila muqawama, Israel ingeshambulia Syria kwa maelfu ya kilomita, na hata kuingilia nchi zingine za Kiarabu bila kizuizi.”

Mwisho

Kuendelea kwa njia ya muqawama wa Hizbullah licha ya kupoteza viongozi na makamanda, hususan shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, si jambo jipya katika historia ya karne ya sasa. Iran pia baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ilipita mitihani sawa wakati wa vita vya kulazimishwa.

Kwa hiyo, wafuasi wa Hizbullah waliolelewa katika shule ya “Seyyid wa Muqawama” wanaelewa vyema kuwa heshima yao ipo katika kuendeleza njia ya muqawama. Huu sio muundo unaotegemea mtu, bali ni imani ya ushindi wa damu juu ya upanga.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha