Sala ya Ijumaa ya tarehe 25 Septemba 2026 imefanyika katika Hawza Imam Ridha (as), Ikwiriri, Mkoa wa Pwani, ikishirikisha wanafunzi, walimu na waumini wanawake na wanaume. Khutba imeangazia fadhila za siku ya Ijumaa, umuhimu wa Sala ya Ijumaa, kujenga uhusiano na Mwenyezi Mungu, kuhuisha imani na kuimarisha umoja wa Kiislamu.
Mwandishi wa safu wa gazeti la The Guardian, Mustafa Bayoumi, amesema kuwa chuki dhidi ya Uislamu nchini Marekani imeendelea kuwa sehemu ya siasa za nchi hiyo, huku tafiti zikionyesha kuwa ongezeko la matamshi na vitendo vya chuki dhidi ya Waislamu mara nyingi huhusishwa zaidi na vipindi vya uchaguzi kuliko matukio ya kigaidi.