8 Septemba 2025 - 13:24
Kozi zenye Mada Maalum | “Misingi ya Itifaki na Ustaarabu”, "Dhana, Historia, Dira, Dhima na Hadhi ya JMAT", Na Zingine Zitatolewa kupitia JMAT

Lengo kuu la kozi hizi ni kuwajengea washiriki uwezo wa kuwa mabalozi wa maadili, ustaarabu na mawasiliano bora katika jamii na katika nafasi zao za kazi au uongozi.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam, Tanzania - Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) imetangaza kuanza kwa kozi maalum ya mafunzo Muhimu kama vile: "Misingi ya Itifaki na Ustaarabu" n.k, itakayofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 18 Septemba, 2025 katika ukumbi wa Nefaland Hotel Hall, uliopo Manzese Argentina, Dar es Salaam.

Kozi hii itakuwa ya siku tatu mfululizo, ikiendeshwa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni kila siku.

Katika kozi hii muhimu, washiriki watafundishwa na wataalam na wakufunzi mahiri kutoka ndani na nje ya nchi, ambao wana uzoefu mkubwa katika masuala ya itifaki, mawasiliano rasmi, maadili ya kijamii na ustaarabu wa kimataifa.

Mada mbalimbali zitajadiliwa kama ilivyoashiriwa hapo juu, ambazo ni pamoja na mada kuhusu: Misingi ya Itifaki na Ustaarabu, "Dhana, Historia, Dira, Dhima na Hadhi ya JMAT".

Lengo kuu la kozi hizi ni kuwajengea washiriki uwezo wa kuwa mabalozi wa maadili, ustaarabu na mawasiliano bora katika jamii na katika nafasi zao za kazi au uongozi.

JMAT inawaalika vijana, viongozi wa dini na jamii, wanafunzi, watumishi wa taasisi mbalimbali na watu wote wenye nia ya kujifunza na kuboresha mienendo yao ya kijamii na kitaasisi kushiriki katika mafunzo haya.

Kwa taarifa zaidi au usajili, tafadhali wasiliana na waandaaji kupitia nambari rasmi za JMAT.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha