Darsa hii imelenga kuwaongezea wanafunzi uelewa wa kina kuhusu wajibu wao wa kisharia katika kushughulikia maiti kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Darsa maalumu ya Ahkaam za Kivitendo imefanyika siku ya Jumamosi tarehe 13 Desemba 2025 katika Msikiti (Eneo la Sala) wa Shule (Hawzat) ya Al-Hadi, nchini Malawi, kuanzia saa 11:00 za jioni hadi 12:00 jioni.
Darsa hiyo ilitolewa na Sheikh Abdulrashid Shu’aib, na ilihudhuriwa na wanafunzi wote wa kidini (Tullab) wa shule hiyo yenye kutoa ilmu na maarifa Matukufu ya Kiislamu.
Mada ya Darsa
Ahkaam za Maiti
Sheikh Abdulrashid Shu’aib aliwafundisha wanafunzi kwa kina masuala muhimu yanayohusiana na:
- 1_Ghusl ya Maiti
- 2_Kafan
- 3_Swala ya Maiti
- 4_Maziko

Hoja Muhimu Zilizojadiliwa
Masharti ya Jumla ya Ghusl ya Maiti
- Uislamu wa Maiti: Ghusl ni wajibu kwa maiti Muislamu.
- Usafi wa Maji: Maji yawe safi na halali (maji mutlaq).
- Utaratibu wa Kisharia: Ghusl ifanywe kwa mpangilio uliowekwa.
- Nia: Mtoa ghusl awe na nia ya ibada (qurbatan ilallah).
- Kufanywa na Binadamu: Ghusl ifanywe na mtu, si kwa mashine.
- Ulinganifu wa Jinsia: Mtoa ghusl na maiti wawe wa jinsia moja, isipokuwa katika hali maalumu kama wanandoa au maharimu.
- Kuondoa Najasa: Najasa iondolewe kabla ya kuanza ghusl.
Namna ya Kufanya Ghusl ya Maiti
- Kuosha kichwa na shingo
- Kuosha upande wa kulia wa mwili
- Kuosha upande wa kushoto wa mwili
Aina za Maji Yanayotumika Katika Ghusl
- Maji yaliyochanganywa na Sidr
- Maji yaliyochanganywa na Kafur
- Maji mutlaq (safi bila mchanganyiko)
Darsa hii imelenga kuwaongezea wanafunzi uelewa wa kina kuhusu wajibu wao wa kisharia katika kushughulikia maiti kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.

Your Comment