Asubuhi
-
IRGC Yatangaza Mashambulizi ya Kulipiza Kisasi Dhidi ya Kambi ya Marekani
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limesema limelenga kambi ya kijeshi ya Marekani baada ya shambulizi lililoripotiwa kufanywa karibu na Uwanja wa Ndege wa Bandar Abbas, likionya kuwa uchokozi wowote dhidi ya Iran utakabiliwa na majibu makali zaidi.
-
Katika siku ya mwisho ya likizo ya Hanuka kilichotokea ni;
Walowezi wa Kizayuni kuuvamia Msikiti wa Al-Aqsa
Walowezi wa Kizayuni leo asubuhi, siku ya Jumatatu, kwa ulinzi na msaada wa majeshi ya uvamizi wa Israel, waliuvamia ua wa Msikiti wa Al-Aqsa.
-
Jeshi la Israel wafanya mashambulizi mapya Gaza baada ya siku ya mauaji makubwa
Jeshi la Israel limefanya mashambulizi ya anga mashariki mwa Khan Yunis na kuua na kuwajeruhi makumi ya raia. Vikosi vya uokoaji viliopoa miili ya mashahidi na kuwahamisha waliojeruhiwa, huku hospitali zikithibitisha vifo 28, wakiwemo watoto 17.
-
Shirika la Kiislamu la Myanmar limeonyesha shukrani zake kwa Mashia kutokana na mchango wao katika kukuza maelewano kati ya dini tofauti
Katika hafla iliyofanyika asubuhi ya jana katika Hoteli ya Central Yangon, Myanmar, Taasisi ya Kiislamu ya Al-Azhar ya nchi hiyo ilitoa shukrani zake kwa wanachama wa jamii ya Shia kutokana na mchango wao katika kuimarisha mshikamano wa amani na maelewano kati ya Waislamu, pamoja na kukuza urafiki kati ya dini na tamaduni tofauti. Hujjatul-Islam Haji Masoom Ali alikabidhiwa Tuzo Maalumu ya Taasisi hiyo kwa niaba ya jamii ya Shia ya jiji la Yangon.
-
Katika kikao na waandaaji wa kongamano la Mirza Naeini,
Kiongozi wa Mapinduzi amesema: Ubunifu wa kielimu na fikra za kisiasa ndizo sifa mbili mashuhuri za Allamah Naeini
Matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alipokutana na washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Allamah Mirza Na'ini yamechapishwa leo asubuhi katika ukumbi wa mkutano huo mjini Qom.
-
Ushambulizi wa wanajeshi wa Israeli dhidi ya nyumba za waliokuwa mateka waliotolewa huru katika Ukingo wa Magharibi
Vikosi vya kikoloni vilivamia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi usiku wa jana na asubuhi ya leo, na kufanya ukaguzi wa nyumba za baadhi ya waliokuwa mateka waliotolewa huru.