19 Aprili 2025 - 22:29
Ni ipi maana ya Meditation (Tafakuri - Kutafakari)?. Je, ni Dini au sio Dini? Samahat Sheikh Dr. Abdur-Razak Amiri anafafanua zaidi kuhusu hilo

"Meditation" ni aina fulani ya utaratibu unaofuatwa Duniani kote sasa hivi. Na baadhi ya watu ili waweze kutafuta namna fulani ya kupumzika na kupunguza shinikizo na mifadhaiko yao, ili wajisikie vizuri na kutibu baadhi ya maradhi ya kisaikoloji, huonekana wakifanya kitu hicho kinachoitwa Meditation.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Samahat Sheikh Dr. Abdur-Razak Amiri akijibu swali aliloulizwa kuhusiana na Meditation ( Uwazo au hali ya Kutafakari), kwamba je inaruhusiwa katika upande wa Dini Tukufu ya Kiislamu amesema: Suala la "Meditation" ni aina fulani ya utaratibu unaofuatwa Duniani kote sasa hivi. Na baadhi ya watu ili waweze kutafuta namna fulani ya kupumzika na kupunguza shinikizo na mifadhaiko yao, ili wajisikie vizuri na kutibu baadhi ya maradhi ya kisaikoloji, huonekana wakifanya kitu hicho kinachoitwa Meditation. Kuna njia nyingi za kutibu maradhi hayo ya Kisaikolojia, moja wapo ni kufanya hiyo harakati ya Meditation. Watu wa maeneo ya Asia na Mashariki ya mbali, ni maarufu zaidi katika kutibu matatizo ya kisaikolojia kwa njia hii na utaratibu huu wa kufanya Meditation. Sasa, swali kwamba hiyo ni ibada au sio ibada, linabakia kuwa ni suala la mjadala".

Samahat Sheikh, aliendedelea kubainisha suala la meditation kwa kutoa mifano zaidi, akisema: "Moja katika namna za kufanya Meditation, ni kuzuia pumzi yako kwa dakika kadhaa, kisha ukaiachia taratibu. Kwa maana mtu anafundishwa kwamba tatizo lako hili, ili uweze kujitibu, ukiamka asubuhi na mapema, au kabla hujalala, basi hakikisha kitu cha kwanza unachokifanya ni kukaa mahala fulani kwa muda wa dakika kumi mpaka kumi na tano, kisha uvute pumzi yako kwa ndani mpaka mwisho kabisa, na ukisha fikia mwisho, anza kuitoa pumzi hiyo taratibu, na wakati huo kwa mujibu wa mafunzo, unaambiwa ufikirie chochote kile, ila suala hilo tu la kuvuta pumzi ndani na kuiachia taratibu. Hiyo ni moja ya utaratibu na aina za Meditation, kwa maana kwamba: Kuna aina kadhaa na tofauti za Meditation / Kutafakari. Kwa ibara nyingine: Meditation ni (Kitendo cha Kutafakari kwa kina, na  kuzingatia jambo moja tu kama njia moja wapo ya kupumzika na kujiletea utulivu wa nafsi. Kwa ibara nyingine: Meditation / Kutafakari ni mwendo na harakati ya kiakili na kimwili ambao mtu huitumia kujitenga na mawazo - fikra - na hisia zake zingine, na kuzingia fikra moja, ili kujiweka katika hali ufahamu na utambuzi kikamilifu). Watu wengi wanaofanya Meditation kwa utaratibu huu, wanaweza kutumia muda mrefu karibia saa moja, na baada ya kufanya hivyo, wanakwambia kuwa wanajisikia raha mstarehe".

Wengine (kwa sababu ya kuitumia vibaya Meditation na kupotoka), wanafikia hatua ya kuacha mpaka Swala kabisa, na kujiingiza zaidi katika suala hili la Meditation, na hoja yao ukiwauliza wanasema kuwa wanaposwali hawaipati ile raha na radha wanayoipata pindi wanapofanya Meditation!. Huu ni mtihani mkubwa, na kwa hakika hivi sasa Arusha kuna mtihani huu wa Meditation! Vipo vitengo vingi Jijini Arusha vinavyojihusisha na suala hili la Meditation. Suala hili Meditation linahusika vipi na mambo ya "Energy in Human Body" / Nishati katika mwili wa binadamu?!.

Hilo linahitajia ufafanuzi na maelezo marefu, lakini kwa kuashiria inasemwa na wataalamu kwamba asubuhi, kuna Energy / Nishati ambayo ni Positive (Chanya), kwa maana kwamba: Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameweka - "Energy" - Nishati / Nguvu katika mazingira yetu ya asubuhi ambayo ni nguvu nzuri na chanya. Sasa wengine wanaofanya Meditation wanasema kwamba: Unapofanya Tafakuri (Meditation) ya asubuhi kwa muda wa dakika 5 au 10, unavuna nguvu (nishati) hiyo ambayo ni nguvu chanya (Positive Energy), kwa maana kwamba baada ya kufanya hivyo nyakati za asubuhi, basi unajihisi kuwa umejaa nguvu chanya mwilini mwako. Kiujumla: Unapoamka asubuhi, hakuna kitu bora kuliko kujihisi kuwa una nishati (nguvu) ya asili katika mwili wako, na kuwa tayari kuianza siku yako mpya. Kuna "Negative and Positive Energy" / (Nishati - Nguvu - Hasi na Chanya). Na kuna namna na jinsi ya kutambua "Nishati - Nguvu - Hasi na Chanya" katika mwili wako. Kila mtu kwa wakati wake anaweza kufanya utafiti ni namna gani ya kuzitambua nguvu hizo mbili (hasi na chanya) katika Mwili wa Binadamu.

Suala la msingi hapa ni hili: Harakati hii ya Meditation, kwa aina yoyote ile utakavyoofanya, ni dini au sio dini?. Kwa hakika, wapo watu wenye dini fulani (kama Dini ya Uhindu, Ubudha, Uyahudi n.k) wanafanya Meditation, lakini wakiichukulia kuwa ni sehemu ya utaratibu wao wa kidini na kiibada, kwa maana Meditation kwao hawaichukulii kuwa ni kwa ajili ya kujiletea pumziko la mwili na utulivu wa nafsi, na kutibu matatizo ya mifadhaiko na kisaikoloji, bali wanaenda mbali zaidi na kuichukulia kuwa ni sehemu ya utaratibu wao wa kidini na kiibada.

Ni ipi maana ya Meditation (Tafakuri - Kutafakari)?. Je, ni Dini au sio Dini? Samahat Sheikh Dr. Abdur-Razak Amiri anafafanua zaidi kuhusu hilo

Na kuna Waislamu wameingia katika suala la Meditation, lakini sio kwa malengo hasi ya kuabudu na kuifanya ni aina moja wapo ya ibada zisizokubalika kwa mujibu wa Dini Tukufu ya Kiislamu, bali wanafanya Meditation kwa malengo chanya ya kupata hicho kinachopatikana ndani ya Meditation (kama vile kupata nguvu chanya ya mwili) n.k".

Mwisho, Samahat Sheikh Dr. Abdur - Razak Amiri ametoa natija ya ufafanuzi wake akisema: Ikithibitika Kisayansi, kwamba mtu (akizuia) akivuta pumzika yake kwa ndani, kisha akaichia taratibu, kuna mambo fulani yatakaa sawa sawa katika mwili wake kiafya, basi kwa hakika jambo hilo litafaa kwa misingi ya Kisayansi. Kwa sababu katika Sayansi imethibitika kuwa: Moja ya njia za kufuta mafaili mabaya katika - Subconscious Mind - Akili ya Chini ya Fahamu ya mtu ni kufanya Meditation".

Kwa faida zaidi: Akili ya chini ya Fahamu - (Subconscious Mind) -  yenye kuhifadhi mafaili mbalimbbali mazuri na mabaya ndani ya ubongo wa Mwanadamu -  ina nguvu zaidi kuliko - (Conscious Mind) -  Akili ya Fahamu (au Akili ya Ufahamu), kwa sababu inaweza kuchakata habari nyingi sana zinazokufikia kupitia hisi zako kuu tano za fahamu (Utambuzi) - Kunusa, Kuonja, Kusikia, Kuona, na Kugusa -  na kisha kuzitafsiri kwenye ubongo wako kwa kufumba na kufumbua. Wataalamu wanasema kwamba Akili hiyo ya Chini ya Fahamu (Subconscious Mind) ina nguvu mara milioni zaidi ya Akili Fahamu - (Conscious Mind).

Akili ya Chini ya fahamu (Subconscious Mind), au kwa ibara nyingine "Akili isiyo na Fahamu," ndio chanzo kikuu cha mwenendo na tabia ya Mwanadamu, na - Akili hiyo ya chini ya Fahamu - ndio sehemu muhimu zaidi ya Akili ya Mwanadamu. Kwa hivyo, tunaweza kusema kuwa ni Akili ya Chini ya Fahamu (Subconscious Mind) ni mgodi wa hisia, mawazo, matamanio, na kumbukumbu nje ya Akili ya Ufahamu (Conscious Mind) . Na ni vyema kutambua sehemu hii kwamba: Inasemwa kuwa mengi ya yaliyomo ndani ya Akili ya Chini ya Fahamu (Subconscious Mind) ni hisia hasi (mafaili mabaya), kama vile: Mtu kuwa na Hisia za Maumivu, Wasiwasi, au Mapambano na misukosuko yake katika maisha, au kurudi nyuma kwenye mawazo mabaya yanayotokana na ule uzoefu uliopita katika maisha yake.

Ni ipi maana ya Meditation (Tafakuri - Kutafakari)?. Je, ni Dini au sio Dini? Samahat Sheikh Dr. Abdur-Razak Amiri anafafanua zaidi kuhusu hilo

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha