Nishati
-
Iran: Baghai Amshutumu Grossi kwa Kudhoofisha Uaminifu wa IAEA
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baghai, amemshutumu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, kwa kutumia ripoti za kitaalamu za wakala huo katika muktadha wa kisiasa, akidai kuwa hali hiyo inahatarisha uaminifu, uhuru na kutokuegemea upande wowote kwa taasisi hiyo.
-
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Nyuklia Iran Awapongeza Viongozi Wapya wa Kijeshi kwa Uteuzi Wao
Mohammad Eslami amewatumia salamu za pongezi viongozi sita wapya wa ngazi za juu katika Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akiwatakia mafanikio katika majukumu yao mapya.
-
Rais Pezeshkian Atoa Wito wa Kudhibiti Matumizi ya Nishati Ili Kuepusha Migogoro
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amesisitiza umuhimu wa kupunguza na kusimamia matumizi ya nishati kama njia kuu ya kuzuia migogoro ya nishati, huku akipendekeza matumizi ya nishati ya jua katika shule.
-
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Auliza: “Yuko Wapi Grossi?” Baada ya Mashambulizi ya Marekani Dhidi ya Vituo vya Nyuklia vya Iran
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baghaei, amekosoa ukimya wa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), Rafael Grossi, kuhusu mashambulizi na vitisho vya Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, akisema mashambulizi hayo ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na kanuni za IAEA.
-
Ismail Baghaei:
Vitisho na Mashambulizi ya Marekani Dhidi ya Vituo vya Nyuklia vya Amani vya Iran ni Ushahidi wa Uadui wa Kina Dhidi ya Sayansi na Maendeleo ya Iran
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Ismail Baghaei, amesema kuwa mashambulizi na vitisho vinavyorudiwa vya Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya amani vya Iran vinaonyesha uadui wa kina wa Marekani dhidi ya sayansi, maarifa na maendeleo ya Iran.
-
Nchi Wanachama wa D-8 Zakubaliana Kupanua Ushirikiano wa Nishati Kupitia Azimio la Baku
Mawaziri na wawakilishi wa nchi wanachama wa D-8 wamepitisha Azimio la Baku, wakisisitiza kuimarisha ushirikiano katika usalama wa nishati, nishati jadidifu na maendeleo ya miundombinu ya pamoja ili kukabiliana na changamoto za sasa za sekta ya nishati duniani.
-
Marekani Yakabiliwa na Shinikizo la Gharama za Maisha, Onyo la Mgogoro wa Chakula Latolewa
Kupanda kwa bei za vyakula, nishati na huduma muhimu kumeongeza mzigo kwa familia nyingi za Marekani, huku wachambuzi wakionya kuhusu hatari ya kuongezeka kwa changamoto za usalama wa chakula na gharama za maisha, jambo linalozidisha mjadala kuhusu mustakabali wa “Ndoto ya Marekani” katika mazingira ya hali ngumu ya kiuchumi.
-
Iraq: Hatutaacha urutubishaji wa urani
Iran haitakoma kurutubisha urani; ni haki yake kama taifa huru, shughuli zote zikiwa salama na zikifuatiliwa na IAEA, na mazungumzo na Marekani yanaendelea bila kujadiliwa kwenye vyombo vya habari.
-
Urusi Yatengeneza Njiwa-Droni Wenye Chipu za Ubongo
Bio-drones za Nairi Group zazua hofu za kijeshi kwa teknolojia ya udhibiti wa neva
-
Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran lafichua mafanikio matatu makubwa ya nyuklia
Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran limetangaza mafanikio matatu makubwa ya nyuklia: kuzindua kichochezi cha kwanza cha viwandani kilichotengenezwa ndani ya nchi, kuanza uzalishaji wa hali ya juu wa Carbon-13, na kurejesha cyclotron kwa ajili ya uzalishaji wa dawa za mionzi licha ya vikwazo.
-
Rais Dkt. Pezeshkian azuru Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran na kupongeza mafanikio ya wanasayansi wa sekta ya nyuklia katika huduma za afya
Rais alisema: “Mafanikio haya ni uthibitisho wa uwezo wa vijana na wataalamu wa Kiirani ambao, licha ya vikwazo vya kigeni, wameweza kuendeleza miradi mikubwa ya nyuklia kwa manufaa ya mwanadamu.”
-
Sayyid Ali Khomeini: “Kama Ubalozi wa Marekani usingelivamiwa, leo tusingekuwa na Makombora wala ishati ya nyuklia"
Akiisisitizia kauli kwamba “uvamizi wa ubalozi wa Marekani uliimarisha uhuru wa Iran,” alisema: “Kama tukio hilo lisingetokea, leo hii Jamhuri ya Kiislamu isingekuwepo, na nchi yetu isingepata teknolojia ya makombora na nishati ya nyuklia, kwani Marekani ilikuwa inapinga maendeleo haya.”