Muqawama
-
Maadhimisho ya Mwaka wa kwanza wa Shahada ya Sayyid Hassan Nasrallah yatafanyika Siku ya Alhamisi
Baraza la Kuratibu Tablighi la Kiislamu limetangaza katika taarifa yake kwamba maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa kifo cha shahidi Sayyid Hassan Nasrallah yatafanyika Alhamisi, tarehe 02 Oktoba, 2025, katika nchi nzima, chini ya kauli mbiu kuu “Innā ‘ala al-‘Ahd”. Hafla kuu itafanyika saa 4:00 usiku katika Uwanja wa Ibada wa Imam Hussein (a.s) mjini Teheran.
-
Profesa kutoka Lebanon katika mahojiano na ABNA:
Jina la Nasrallah limehusishwa na usalama na uaminifu / Silaha za Hezbollah zitaendelea kuwa sehemu ya mlingano wa Lebanon na eneo la kikanda
Yeye (Sayyid Hassan Nasrallah) alihesabiwa kuwa alama ya heshima na mapambano kwa wote, na alikuwa mfano wa malengo ya sehemu kubwa ya wapiganaji wa muqawama wa Kishia ambao kwa vitendo walitaka kufikia mamlaka, uhuru, na kujitegemea kwa Lebanon.
-
Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu wa Bahrain:
Kujiondoa kwenye njia ya Muqawama (Mapambano ya kupinga dhulma) ni sawa na fedheha na udhalili
Mwenyekiti wa Baraza la Wanazuoni wa Kiislamu wa Bahrain alisisitiza kuwa kuacha njia ya Muqawama (mapambano dhidi ya wavamizi na dhulma) hakuzai chochote isipokuwa fedheha, udhalilishaji na utumwa.
-
Mtazamo juu ya Septemba ya Umwagaji Damu Lebanon;Kuanzia Jinai za Pagers hadi Subira ya Kistratejia ya Hizbullah baada ya Shahidi “Sayyid wa Muqawama"
Siku hizi ni kumbukumbu ya jinai za kipekee za utawala wa Kizayuni nchini Lebanon – kuanzia milipuko ya pageri hadi mauaji ya makamanda waandamizi wa Hizbullah. Hivyo basi, Septemba ya mwaka uliopita kwa Wana-Lebanon imekuwa mwezi usiosahaulika
-
Atlantic: Iran Yajenga Njia Mpya na Kuwapita Maadui Zake
Tabia ya ustahimilivu ya Iran na mhimili wa muqawama (mapambano ya upinzani) katika miongo iliyopita imeonyesha kuwa, licha ya mashinikizo na mashambulizi kutoka Marekani na utawala wa Kizayuni, Iran daima imeweza kujirekebisha kimkakati na kupata njia mpya za kukabiliana na changamoto.
-
Katibu Mkuu wa Hizbullah: Kama siyo Muqawama, Israel ingeingia Beirut / Kamwe hatutaweka silaha chini
Sheikh Qasim alieleza kuwa ramani ya njia ya baadaye ni: kufukuza adui kutoka ardhi ya Lebanon, kusimamisha uvamizi, kuwaachia huru wafungwa, kuanza upya ujenzi wa taifa na kisha kushughulika na mkakati wa ulinzi wa kitaifa.
-
Maandamano Makubwa ya Wenyeji Lebanon Kupinga Uamuzi wa Serikali wa Kuvunja Silaha za Muqawama
Wananchi wa maeneo mbalimbali ya Lebanon wamefanya maandamano na mikutano ya hadhara kupinga uamuzi wa serikali wa kuhodhi na kuvunja silaha za vikosi vya Muqawama.