23 Februari 2026 - 20:41
Upendo na Uaminifu Usio na Kikomo kwa Muqawama na Wilayat; Kumbukumbu ya Mashahidi Nasrallah na Safiyyu al-Din

Katika kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa mazishi ya mashahidi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah na Hashim Safiyyu al-Din, Naim Qassem alisisitiza kuendelea kwa njia ya Muqawama na uaminifu (Wilayat) kwa Kiongozi Sayyid Ali Khamenei, akieleza kuwa Muqawama hauwezi kushindwa iwe kwa ushindi au kwa shahada.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika maadhimisho ya mwaka wa kwanza tangu mazishi ya heshima ya mashahidi wawili mashuhuri wa Hezbollah - Hassan Nasrallah na Hashem Safieddine - Naim Qassem katika mahojiano na chombo cha habari cha Al-Ahed alifufua kumbukumbu za siku hiyo ya kihistoria, na kusifu mapenzi na uaminifu wa kina wa viongozi hao kwa Ali Khamenei na harakati za muqawama.

Sheikh Naim, akirejelea maisha na huduma zao, alimuelezea Sayyid Hassan Nasrallah kama “mlima ulioinuka juu angani,” na Sayyid Hashem Safi al-Din kama “nguzo ya muqawama,” akisisitiza kuwa njia yao inaendelea na kwamba Muqawama, iwe kupitia ushindi au kupitia shahada, Huawezi kushindwa.

Ukumbusho huu wa kihistoria umeonyesha si tu mapenzi ya kibinafsi bali pia uaminifu wa pamoja kwa muqawama, msimamo thabiti mbele ya adui, na mshikamano kati ya viongozi hao na wananchi wa Lebanon. Pia umetuma ujumbe wazi kwa dunia kuhusu mwendelezo wa njia ya muqawama na kujitolea kwa kizazi kipya katika kushikamana na maadili na malengo ya mashahidi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha