29 Julai 2026 - 21:05
Tukio la Tatu la Kimataifa la “Sisi ni Wana wa Hussein (as)”

Wito kwa wanahabari, watayarishaji wa maudhui na wadau wa vyombo vya habari kushiriki katika kampeni ya kurekodi na kuhifadhi mandhari mbalimbali za Arbaeen ya Imam Hussein (as). Washiriki wanakaribishwa kutuma kazi katika nyanja za picha, video, maudhui ya Akili Bandia (AI) na podcast, zikiwemo mada maalumu kuhusu Kiongozi Shahidi katika njia ya Hussein (as) na Dunia moja katika kumbatio la Hussein (as). Kazi zinapaswa kutumwa kupitia @nahno_abna_alhussain kabla ya 22 Septemba 2026.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Lifuatalo ni Tangazo la: Wito wa kushiriki katika Kampeni ya utayarishaji wa maudhui ya vyombo vya Habari kwa lengo la kurekodi na kuhifadhi mandhari mbalimbali za Arbaeen ya Imam Hussein (as).

Katika vipengele vifuatavyo:

Picha (za kitaalamu, za simu na mkusanyiko wa picha)

Video (za taarifa, za makala na vlog)

Akili Bandia (picha, video na sauti)

Podcast
Sehemu maalumu:

🔹 Kiongozi wetu, Shahidi, katika njia ya Hussein (as)
(Kurekodi Mandhari za mapenzi na heshima ya wageni wa Arbaeen kwa Kiongozi Shahidi)

🔹 Dunia moja katika kumbatio la Hussein (as)
(Kurekodi mandhari za uwepo wa wageni wa kimataifa na bendera za nchi mbalimbali)

Njia za mawasiliano kwa ajili ya kutuma kazi:

@nahno_abna_alhussain

Mwisho wa kutuma kazi:
22 Septemba 2026

Tukio la Tatu la Kimataifa la “Sisi ni Wana wa Hussein (as)”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha